Naibu waziri Ofisi ya Raisi TAMISEMI Mhe. Josephat Kandege ameridhishwa na matumizi ya fedha kwenye ujenzi na uboreshaji wa Kituo cha Afya Usa- River na kueleza kuwa thamani ya fedha imeonekana pia ametoa wito kwa Halmashauri nyingine kuiga mfano.
Mhe.Naibu Waziri Kandege amesema hayo alipokagua ujenzi na ukarabati wa kituo cha Afya Usa- River wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa vituo vya Afya vilivyopewa fedha na Serikali kwenye Mkoa wa Arusha kwaajili ya ujenzi wa majengo mapya na kukarabati yaliyopo kwa lengo la kutoa huduma bora za Afya, pia Mhe.Naibu Waziri Kandege amemwagiza Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Dkt. Cosmas Kilasara kutoa elimu ya kina kwa wananchi ili waweze kujiunga na mfuko wa Afya ya jamii CHF.
Aidha ujenzi wa miundombinu mbalimbali kwenye kituo hicho cha Afya Usa -River ni baada ya Serikali kutoa fedha kiasi cha Sh. milioni 500 kwa ajili ya kuboresha kituo hicho kwa kujenga majengo mapya ambayo ni jengo la maabara,nyumba ya mtumishi, jengo la upasuaji, wodi ya mama na mtoto, chumba cha kuifadhia maiti, kichomea taka pamoja na kufanya ukarabati wa majengo yaliyokuwepo kwa lengo la kuwapa wananchi huduma bora za afya na kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.
PICHA ZA TUKIO.
Naibu waziri Ofisi ya Raisi TAMISEM mhe. Josephat Kandege(wakwanza kulia) akiwa na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu Tawala wa Wilaya ya Arumeru, Ndg.Timotheo Mzava,Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Ndg.Christopher Kazeri,Mganga mkuu wa Mkoa wa Arusha Dkt. Timoth Wonanji ,Mganga mkuu wa Halmashauri ya Meru Dkt. Cosmas Kilasara pamoja na wataalamu wenginewakitembelea na kukagua ujenzi kwenye kituo cha Afya Usa-River.
Naibu waziri Ofisi ya Raisi TAMISEM mhe. Josephat Kandege alipotembelea jengo la Upasuaji kwenye kituo cha Afya Usa-River.
Naibu waziri Ofisi ya Raisi TAMISEM mhe. Josephat Kandege alipotembelea jengo la Upasuaji kwenye kituo cha Afya Usa-River.
Naibu waziri Ofisi ya Raisi TAMISEM mhe. Josephat Kandege alipotembelea jengo la kuwahudumia wagonjwa wa wa nje (OPD)
Naibu waziri Ofisi ya Raisi TAMISEM mhe. Josephat Kandege alipotembelea jengo la kuwahudumia wagonjwa wa wa nje (OPD)
Naibu waziri Ofisi ya Raisi TAMISEM mhe. Josephat Kandege alipotembelea jengo la wodi ya mama na mtoto kwenye kituo cha Afya Usa-River.
Naibu waziri Ofisi ya Raisi TAMISEM mhe. Josephat Kandege alipotembelea sehemu ya kufulia iliyopo kwenye wodi ya mama na mtoto kwenye kituo cha Afya Usa-River.
Naibu waziri Ofisi ya Raisi TAMISEM mhe. Josephat Kandege alipotembelea kichomea taka katika Kituo cha Afya Usa-River.
Naibu waziri Ofisi ya Raisi TAMISEM mhe. Josephat Kandege akikagua upauzi wa njia ya kuptia wagonjwa .
Naibu waziri Ofisi ya Raisi TAMISEM mhe. Josephat Kandege akitoa mrejesho wa ukaguzi wa kituo cha Afya Usa-River.
Naibu waziri Ofisi ya Raisi TAMISEM mhe. Josephat Kandege akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Christopher Kazeri .
PICHA ZA MAJENGO.
Jengo la wodi ya Mama na Mtoto litapunguza vifovitokanavyo na uzazi pamoja na msongamano wa wagonjwa kwenye Hospitali yaWilaya.
Jengo la upasuaji pindi litakapoanza kutumika kwa kiasi kikubwa litapunguza vifovitokanavyo na uzazi pamoja na msongamano wa wagonjwa kwenye Hospitali yaWilaya.
Nyumba ya mtumishi itaboresha mazingira ya mtumishi kufanya kazi kwenye mazingira rafiki hivyo huduma za dharura kupatikana kwa urahisi.
Jengo la kuhifadhia maiti .
Jengo la duka la dawa ambalo awali lilitumika kama kama jengo la maabara.
Mwonekano wa ndani wa chumba cha upasuaji.
Mwonekano wa ndani kwenye jengo la wodi ya mama na mtoto.
Sehemuya kufulia kwenye Jengo la wodi ya Mama na Mtoto ikiwa na uhakika waupatikanaji wa maji wakati wote kutokana na uwepo wa matanki ya kuifadhia maji.
Mwonekano wa ndani kwenye sehemu ya kufulia kwenye jengo la mama na mtoto.
Picha ya kichomea taka kipya kwenye kituo cha Afya Usa-RIVER.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa