Halmashauri ya Wilaya ya Meru ilipokea shilingi 177,765,163.33.00 kutoka TASAF makao makuu kwa ajili ya Malipo na Usimamizi wa malipo hayo kwa walengwa 5,553 wa Mpango wa kunusuru kaya maskini katika vijiji 47 kwa kipindi cha Julai/Agosti 2017.
Kiasi cha shilingi 164,580,000.00 kati ya kiasi kilichopokelewa zilikuwa ni kwa ajili ya malipo kwa walengwa na kiasi kilichobakia, yaani shilingi 13,185,163.33 zilikuwa ni kwa ajili ya ajili ya usimamizi wa malipo hayo katika ngazi za vijiji na Halmashauri. Matumizi ya fedha za usimamizi ni pamoja na posho na nauli za wajumbe wa kamati za usimamizi za vijiji, posho za viongozi wa vijiji na wasimamizi wa Halmashauri, gharama za magari pamoja na ulinzi kwa muda wa siku zote za malipo.
Malipo yatafanywa kwa muda wa siku 5 kuanzia Alhamisi tarehe 10/08/2017 hadi Jumatano tarehe 16/08/2017. Hadi zoezi la malipo linakamilika, kaya 5,431 zililipwa jumla ya shilingi 161,104,000.00. Kutokana na malipo hayo, kaya hizi ziliongezewa uwezo wa kifedha wa kukidhi mahitaji mbalimbali katika familia na jamii kwa ujumla.
Kaya 122 zilizostahili kulipwa hazikuweza kulipwa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo vifo na kutojitokeza siku za malipo. Hali hiyo ilisababisha shilingi 3,476,000.00 kubaki, kiasi ambacho kitarejeshwa TASAF makao makuu.
Zoezi la malipo kwa kipindi cha Julai/Agosti lilihitaji usafiri wa magari kwa ajili ya kupeleka wawezeshaji wa Halmashauri vijijini na kuwarudisha mara baada ya malipo. Aidha, usafiri ulihitajika kwa ajili ya kuchukua wajumbe wa kamati za TASAF za vijiji (wawili kila kijiji) pamoja na askari kutoka Benki na kuwapeleka vijijini. Kwa ajumla yalihitajika angalau magari matatu ili kufanikisha zoezi hili. Kwa bahati mbaya yalipatikana magari mawili tu ambapo moja kati ya hayo lilikuwa na majukumu mengine mbali na zoezi la malipo. Hali hii ilisababisha mara nyingine malipo kufanywa hata baada ya muda wa kazi kumalizika.
Muhtasari wa malipo kwa kila kijiji ni kama ilivyoonyeshwa kwenye jedwali hapa chini:
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa