Halmashauri ya Wilaya ya Meru imetoa fedha, kiasi cha shilingi miloni 315 ikiwa ni mkopo usio na riba kwa vikundi 40 vya Wanawake, vikundi 23 vya Vijana, pamoja na vikundi saba vya watu wenye Ulemavu, ikiwa ni utekelezaji wa agizo ya Serikali kwa Halmashauri kuwawezesha wananchi kiuchumi kwa kutoa asilimia 10 % ya mapato yake ya ndani kwa makundi hayo matatu kama mikopo isiyo na riba .
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya utoaji mafunzo na ukabidhi wa hundi ya mfano, iliyofanyika viwanja vya halmashauri hiyo, Bi.Flora Msilu ambaye ni Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii amesema Halmashauri ya Meru inaendelea kutekeleza kwa vitendo, azimio la Serikali ya awamu ya sita la kuwawezesha Wananchi kiuchumi kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri.
Msilu, ametoa Wito kwa wanufaika wa mkopo huo kufanya marejesho ili kutoa fursa kwa wananchi wengine kunufaika , vilevile amehimiza
Wanufaika kutumia mkopo kwa malengo kusudiwa ambapo amehimiza mkopo kuimarisha amani na upendo ndani ya familia.Pia amewakumbusha wazazi/walezi kutenga muda wa kuwasikiliza na kuwahudumia watoto ili kuzuia na kutokomeza vitendo vya kikatili dhidi yao "wazazi tusiwasahau watoto kwa kigezo cha kutafuta fedha" amesisitiza Msilu
Kwa upande wao Viongozi wa Jumuia ya Vijana wa CCM wametoa Wito kwa Vijana kutumia mkopo huo kwa tija ili kujikwamua kiuchumi na kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa Taifa ambapo wamebainisha chama cha mapinduzi kuendelea kuhakikisha Serikali inawaletea wananchi maendeleo "Nitoe Wito kwa Vijana kuchangamkia fursa ya mikopo isiyo nariba ya asilimia 10% kujikwamua kiuchumi na kushiriki kulijenga Taifa"amehimiza Ombeni Elisante Mwenyekiti wa UVCCM Meru
"Chama cha mapinduzi kinahakikisha wananchi mnapata maendeleo utoaji huu wa mkopo usio na riba ni utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Sura ya Pili ibara 23 ambayo inalenga kuwawezesha wanawake ,Vijana na Wenye ulemavu kujikwamua kiuchumi" amefafanua Remmy Nasari katibu wa UVCCM Meru
Ikumbukwe utoaji huu wa Mkopo ni kwa kipindi cha Robo ya Pili ya Mwaka wa Fedha 2022/2023
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa