Afisa uandikishaji jimbo la Arumeru Mashariki Ndg.Emmanuel Mkongo atoa wito kwa wananchi Jimboni humo ambao bado hawajaboresha taarifa zao kwenye daftari la kudumu la mpiga kura na wale ambao watakua na umri wa miaka 18 ifikapo 28 Octoba 2019, kujiandikisha ili wasikose haki yao ya kikatiba ya kushiriki uchaguzi mkuu mwaka 2020.
Mkongo amekumbusha hilo wakati alipokuwa kwenye ufuatiliaji wa namna zoezi la uandikishaji linavyoendelea katika Kata ya Shambarai Burka, Mbuguni na Kikwe.
AidhaMkongo amesisitiza kuwa zimebaki siku 4 tu zoezi la uandikishaji likamilikeJimboni humo, hivyo wananchi wenye sifa wajitokeze kujiandikisha na kupata vitambulisho vya mpiga kura.
Zoezi la uboreshaji daftari la kudumu la mpiga kura Jimbo la Arumeru Mashariki limenza tarehe 18/07/2019 na litakamilia tarehe 24/07/2019.
Zoezi luandikishaji daftari la kudumu la mpiga katika kituo cha kupiga kura Shule mpya Kata ya Shambarai Burka.
Afisa uandikishajimbo la Arumeru Mashariki akipokea maelezo toka kwa mwandishi msaidizi kituo cha kupiga kura Uswahilini Kata ya Kikwe.
Afisa uandikishaji alipotembelea kituo cha kupiga kura katika kitongoji cha Msufini Kata ya Mbuguni.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa