Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru ,Ndg.Emmanuel Mkongo, wakati akifungua mafunzo kwa waandikishaji wa mfuko wa bima ya afya ya jamii iliyoboreshwa iCHF, ametoa wito kwa wananchi wa Halmashauri hiyo kujiunga na bima hiyo ili wawe na uhakika wa huduma za Afya wakati wote .
Mkongo amesema ni muhimu kwa jamii kulipa suala la afya kipaumbele kwani ndio chanzo cha kwanza cha maendeleo ambapo amewataka waandikishaji hao kuzingatia mafunzo hayo kwa makini ili waweze kuifanya kazi hiyo ya uandikishaji kwa ufanisi, "bila nguvukazi ya kutosha inayotokana na afya njema hakuna maendeleo" amesisitiza Mkongo.
Mratibu wa CHF Mkoa wa Arusha,Ndg.Erena Materu mbali na kuipongeza Halmashauri ya Meru kwa kuharakakisha taratibu za uandikishaji wa bima hiyo ya CHF iliyoboreshwa ambapo ni Halmashauri ya pili katika Mkoa huo kutoa mafunzo kwa waandikishaji,ametoa wito kwa Mkuu wa idara ya Afya kuhakikisha pindi mwananchi anapojiunga na mfuko huo anapata huduma kuanzia ngazi ya zahanati.
Naye Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo Dkt.Maneno Focus amefafanua kuwa upatikanaji wa dawa na vifaa tiba katika Halmashauri hiyo ni wa kuridhisha kwani asilimia 90 ya dawa muhimu zinapatikana na ameahidi kuendelea kusimamia vyema upaktikanaji wa huduma za afya kuanzia ngazi za Zahanati.
mmoja wa wawezeshaji wa mafunzo hayo toka Shirika la Pharmaccess International linalofadhili mafunzo hayo,Ndg.Emmanuel Carl ameeleza kuwa Serikali kwa kushirikiana na wadau ilifanya utafiti wa changamoto za CHF ya zamani na kuzitafutia ufumbuzi kwa kuja na mfuko huu wa CHF iliyoboreshwa ambao utakaotoa huduma Nchi nzima .
Carl ameelezea kuna manufaa makubwa kwa Kaya itakayojiunga na mfuko huu wa CHF iliyoboreshwa kwa kuchangia fedha kiasi cha tsh.30.000 ,kwani Kaya hiyo itapata huduma za afya ikihusisha matibabu yote,vipimo ya maabara,uchunguzi kwa njia ya mionzi yaani X-ray na Ultrasound, huduma za afya ya kinywa na huduma za upasuaji zitatolewa katika mfuko huo kwa kufuata taratibu ambapo mwanachama ataanzia Zahanati na kituo cha afya kilichopo karibu nae na ikibainika anahitaji matibabu ngazi nyingine atapewa rufaa kwenda katika Hospitali ya Wilaya au Hospitali ya Rufaa ya Mkoa husika.
Carl Amefafanua kuwa bima ya CHF iliyoboreshwa haitohusika kupata huduma zote zinazohusisha madaktari bingwa wabobezi pamoja na vipimo vinavyotolewa na hospitali za rufaa za kitaifa za kanda .
kwa mujibu wa CHF iliyoboreshwa Kaya ni baba ,mama na watoto wanne wasiozidi umri wa miaka 18 pamoja na mwanakaya mwenye ulemavu ambaye imethibitika hana uwezo wa kujipatia kipato.Pia kwa wanafunzi wa wa Shule za Sekondari na vyuo vya mafunzo stadi taasisi zitahusika kuwaandikishwa wanafunzi wasiozidi 5 kwenye bima ya CHF Iliyoboreshwa.
Mafunzo hayo yanafanyika kwa Siku mbili kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Meru yamejumuisha waandikishaji toka kata 26 za Halmashauri hiyo .
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru,Ndg.Emmanuel Mkongo.
Mratibu wa CHF Mkoa wa Arusha,Ndg.Erena Materu
Mkuu wa Idara ya Afya Halmashauri ya Meru Dkt.Focus Maneno
Mmoja wa wawezeshaji wa mafunzo hayo toka Shirika la Pharmaccess International linalofadhili mafunzo hayo,Ndg.Emmanuel Carl.
Mratibu wa CHF iliyoboreshwa wa Wilaya Tumaini Mayeye
(Kushoto) ni Afisa Tehama Mkoa Obedi Mkuya na kulia kwake ni Steven Kauli Afisa Tehamaa Halmashauri ya Meru.
Maafisa Waandikishaji wa CHF iliyoboreshwa wakati wa mafunzo.
Maafisa Waandikishaji wa CHF iliyoboreshwa wakati wa mafunzo.
Maafisa Waandikishaji wa CHF iliyoboreshwa wakati wa mafunzo.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa