# Ameahidi kuanza na kushughulikia migogoro ya ardhi inayowakabili wananchi na kuwataka Madiwani hao, kuungana na Serikali ya awamu ya tano, kutatua migogoro ya ardhi huku akiwaonya kutokujihusisha na migogoro hiyo kwa maslahi yao binafasi kulingana na nafasi zao katika jamii.
# Amewataka Madiwani kubuni vyanzo vipya vya mapato pamoja na kushiriki kusimamimia ukusanyaji wa mapato katika maeneo yao, ili kuongeza kiwango cha ukusanyaji katika halmashauri hiyo.
# Amethibitisha kuwa ikiwa kutakuwa na usimamizi imara wa ukusanyaji wa mapato, kupitia vyanzo vya mapato vilivyo na kubuni vyanzo vingine vipya, Halmashauri ya Meru, inaweza kukusanya mapato zaidi na kuweza kufiisha kiasi cha shilingi billion kumi kwa mwaka.
#Endapo madiwani hawatashiriki katika usimamizi thabiti waukusanyaji wa mapato, ni dhahiri Halmashauri italazimika kutolipa posho za madiwani hao kutokana na wao kushindwa kutekeleza majukumu yao.
# Amewataka Madiwani kufanya kazi ya kuwatumikia wananchi, kwa weledi kwa kuzingatia kanuni, sheria na taratibu .
..
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa