Aliyekua Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Alexander Mnyeti amewataka watumishi wa Halmashauri ya Meru kushirikiana na kuchapa kazi kuendana na Serikali ya awamu ya Tano na kuwasihi kusamehana pale tofauti zinapotokea ili kuboresha mahusiano yao ya kazi na kuleta tija kwenye utendaji kazi,haya amesema wakati akiagana na watumishi hao kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo ambapo Kaimu mkuu wa Wilaya ya Arumeru ambaye pia ni Mkuua wa Wilaya ya Longido Daniel Chongolo alitambulishwa .
Aidha tarehe Mosi mwezi huu Myeti kwenye kikao maalumu cha viuongozi wa Wilaya ya Arumeru aliwaaga kwa kuwashukuru kwa ushirikiano waliompa na kuwasihi kumpa ushirikiano huo kaimu Mkuu wa Wilaya hiyo Daniel Chongolo.Pia amewasihi viongozi wa vijiji na kata kufanya kazi kwenye mipaka yao ili kumsaidia Danieli Chongolo
Mnyeti Aliipongeza Halmashauri ya Meru kwa kununua pikipiki 26 kama vyombo vya Usafiri kwa Maafisa watendaji wa Kata jambo litakalo boresha utoaji huduma na kukabithi pikipiki hizo kwa Maafisa watendaji wawili wa kata ya Nkoanekoli na Usariver kwa niaba ya wengini pia alimtaka Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Arusha Dkt.. Wilson Mahera Charles kuwanunulia pikipiki Maafisa watendaji wa kata wa Halmashauri hiyo.
Picha ya Maafisa Watendaji wa Kata wanawake wakifurahia pikipiki walizokabithiwa na Halmashauri ya Meru kama vyombo vya usafiri,wa kwanza kushoto ni Afisa Mtendaji wa Kata ya Nkoaneoli Climentina L. Mbise amesema kua Pikipiki hizo zitarahisisha utendaji kazi na kuleta maendeleo kwenye Kata na Viijiji kwani zitatumiwa na wataalamu mbalimbali waliopo kwenye Kata kwenye kutekeleza majukumu yao.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa