Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida amekabidhi rasmi Ofisi kwa Mkuu mpya wa Wilaya ya Arumeru Eng.Richard Ruyango.
Muro amewashukuru Viongozi wa Halmashauri za Arusha na Meru, Kamati ya ulinzi na Usalama, Watumishi wa Wilaya hiyo na Viongozi wa Dini na Mila na Wananchi kwa Ushirikiano waliompa kipindi cha uongozi wake na kuwataka kushirikiana na Mkuu mpya wa Wilaya .
Naye Eng.Richard Ruyango,Mkuu mpya wa Wilaya ya Arumeru ambaye ametokea katika Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera ametoa dira ya Wilaya kuwa itajikita katika ushirikiano wa kutatua changamoto zinazowakabili wananchi ili kuharakisha Maendeleo Wilayani humo.
Eng.Ruyango ameeleza kuwa ataendeleza Yale mazuri yaliyopo Arumeru ambapo amewataka Watumishi kuchapa kazi kwa bidii na kutoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Serekali katika suala la maendeleo.
Aidha, Wakuu hao wa Wilaya wamemshukuru Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuwaamini na kuahidi kumwakilisha vyema kwa kutatua changamoto za Wananchi na kusimamia shughuli za Maendeleo.
Akizungumza kwa niaba ya Wakuu wa Idara na Watumishi wengine wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Marcuz Nazi ambaye ni Mkuu wa Idara ya Elimu Msingi amewapongeza Wakuu hao wa Wilaya kwa kuendelea kuaminika na kuteuliwa katika nyazifa hizo pia ametumia fursa hiyo kumkaribisha Mhe. Eng.Richard Ruyango, Mkuu wa Wilaya ya Arumeru na kumuaga Mhe. Jerry Muro, Mkuu wa Wilaya ya Ikungi.
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro (Kushoto) akimkabidhi rasmi Mkuu mpya wa Wilaya ya Arumeru Eng.Richard Ruyango(kulia).
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Eng.Richard Ruyango akizungumza na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Ndg.Jerry Muro Mkuu wa Wilaya ya Ikungwi akiagana na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Mkurugenzi Mtendaji WA Halmashauri ya Wilaya ya Meru Ndg.Emmmanuel Mkongo wakati WA Ukaribisho WA Mkuu wa Wilaya ya Arumeru.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa