Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru ,Emmanuel Mkongo amethibitisha kupokea barua ya kujiuzulu toka kwa Diwani wa Kata ya Usa-River,Ndg.Hendry B. Mpinga
Henry B. Mpinga amesema hawezi kupinga maendeleo yanayotekelezwa kupitia ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) hivyo amejiuzulu na kumuunga mkono kazi zinazofanywa na Mhe .Rais Dkt.John Joseph Pombe Magufuli katika kuwaletea Watanzania maendeleo.
Hata hivyo amejivua uanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Halmashauri ya Wilaya ya Meru inajumla ya Kata 26 ambapo hadi sasa baraza la Madiwani lina jumla ya Madiwani 25 wakuchaguliwa ambapo Madiwani 14 watokanao na Chama cha CHADEMA NA 11 Wanatokana na Chama cha CCM.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa