• Barua pepe |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
Meru District Council
Meru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Meru

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, Takwimu na Ufatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Utumishi na Utawala
      • Usafi na mazingira
      • Ardhi na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Manunuzi na ugavi
      • Uchaguzi
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Misitu
    • Ufugaji wa Ngombe wa Maziwa
    • Ujenzi wa Kituo cha Biashara
    • Ujenzi wa Eneo la Mapumziko
    • Ujenzi wa kituo cha Mabasi cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Malori cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Michezo
    • Kilimo cha Nyanya
    • Ufugaji wa Nyuki
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • AIDS
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Miongozo
    • Fomu mbalimbali
    • Utaratibu
  • Kituo cha habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

ARUMERU, WADAU WACHANGIA KOMPUTA 580, TEHAMA KWANZA

Imewekwa: September 13th, 2021

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhandisi Richard Ruyango amekabidhi kwa Shule ya Sekondari Sing'isi
kompyuta mpakato 20 ikiwepo Kompyuta Kuu (server)yenye ukubwa wa GB 2000 ambayo imewekewa Vitabu vya ziada na kiada, mitihani ya Kitaifa ya masomo yote toka mwaka 1990 mpaka 2020 kwa ajili ya rejea kwa wanafunzi na walimu, video za masomo mbalimbali   ikiwa ni Sehemu ya Kompyuta 580 zilizotolewa na wadau wa Reneal international Education Outreach Wilayani humo.

Ruyango ametoa wito kwa wadau kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuongeza wigo wa matumizi  sahihi ya TEHAMA katika Shule za Msingi na Sekondari na kuutaka Uongozi wa Shule ya Sekondari Sing'isi kuhakikisha Kompyuta hizo zinatunzwa na kuhifadhiwa vyema  Ili kuwa na  tija iliyokusudiwa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl. Zainabu Makwinya ametoa wito kwa Walimu kutimiza wajibu wao kwani mwalimu ana nafasi  Kubwa ya kumjengea Mwanafunzi msingi thabiti wa kielimu,pia niwakati wa Walimu kujiendeleza katika masomo ya ICT "tuwajengee misingi ya kesho yao" amehimiza Mwl.Makwinya

Kwa upande wake, Mkuu wa Shule ya Sing'isi Mwl.Datus Muganga amesema  walimu na Wanafunzi watanufaika na Kompyuta hizo, kwani zinarahisisha ufundishaji na wanafunzi wanapata fursa ya  kujisomea na kufanya majaribio mbalimbali .

Afisa TEHAMA Mkoa wa Arusha Ndg.David Nyangaka amesema programu ya utoaji wa Kompyuta kwa Shule za Serikali inayofanywa na shirika la Reneal international Education Outreach  imezaa matunda Mkoani humo kwani baadhi ya Halmashauri wanafunzi wamefanya mitihani ya kitaifa  ya ICT na matokeo yanaridhisha.

Diwani wa Kata ya Sing'isi Mhe.Elisa Nassari amesema Kata hiyo itaendelea kuhamasisha wadau kushirikiana nao katika shughuli mbalimbali za maendeleo.

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru akiwasili katika Shule ya Sekondari Sing'isi pamoja na viongozi alioambatana nao.

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Akikabidhi kompyuta kwa mmoja wa Walimu wa Shule ya Sekondari Sing'isi

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Zainabu Makwinya akizungumza na walimu wa Shule ya Sekondari Sing'isi.

Mkuu wa Shule ya Sing'isi Mwl.Datus Muganga akishukuru baada ya kukabidhiwa Kompyuta .

Afisa TEHAMA Mkoa wa Arusha Ndg.David Nyangaka akizungumza wakati wa kukabidhi kompyuta kwa Shule ya Sekondari Sing'isi

Diwani wa Kata ya Sing'isi Mhe.Elisa Nassari akizungumza Katika Shule ya Sekondari Sing'isi

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhandisi Richard Ruyango akizungumza na walimu wa Shule ya Sekondari Sing'isi.

Walimu wa Shule ya Sekondari Sing'isi

Walimu Shule ya Sekondari Sing'isi 




Matangazo ya Kawaida

  • KUITWA KWENYE USAILI October 28, 2024
  • KUITWA KWENYE USAILI June 24, 2024
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MTAALA WA ELIMU YA AWALI NA MSINGI 2022. February 18, 2022
  • UUZAJI WA VIWANJA ENEO LA NGURUDOTO LIMEANZA. November 27, 2018
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • AJIRA MPYA MERU DC WAPATIWA MAFUNZO

    April 02, 2025
  • NAIBU WAZIRI MAENDELEO YA JAMII,JINSIA WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUMU AKAGUA MIRADI YA S.O.S

    March 15, 2025
  • MAFUNZO YA MFUMO WA TAUSI MERU DC YAFUNGWA

    February 15, 2025
  • TAHAPAO NA MERU DC WAWEKA NGUVU KWENYE KAMATI ZA MTAKUWA

    February 19, 2025
  • Tazama Vyote

Video

ELIMU YA KUKABILIANA NA TAHADHARI YA MVUA ZA EL NINO YAANZA KUTOLEWA HALMASHAURI YA MERU.
Video Zaidi

Viungo Haraka

  • Kupata Salary Slip
  • Sheria ndogo za Halmashauri ya Wilaya ya Meru

Kiungo Kuhusiana

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Utumishi
  • Watumishi Portal
  • Tovuti ya Mkoa wa Arusha
  • Ajira Portal
  • Government Salary Slip Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Meru

    Anwani: P.o. Box 462 Usa River

    Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@merudc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa