Halmashauri ya Wilaya ya Meru Wilayani Arumeru leo wamefanya maadhimisho ya Siku ya Usafi wa Mazingira Kitaifa.
Maadhimisho hayo yameongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Emmanuela Kaganda kwa kufanya usafi katika maeneo ya Leganga, Usariver na Makumira kwa kushirikiana na Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl. Zainabu J. Makwinya, Watumishi wa Halmashauri, viongozi mbalimbali, taasisi binafsi na serikali pamoja na wananchi wa maeneo hayo.
Katika kutekeleza zoezi hilo, Mhe. Kaganda amewataka wananchi kuwa na desturi ya kutunza mazingira kwa kufanya Usafi mara kwa mara ili kupunguza mlundikano wa taka katika maeneo yao.
Aidha, Mkuu wa Wilaya hiyo, ametoa maelekezo kwa wale wote wenye maduka na ambao hawakujitokeza kufanya Usafi na maeneo yao kuwa machafu, watozwe faini ya shilingi 50,000. Pia, amesisitiza wananchi kuwa na desturi ya kufanya usafi kwenye maeneo yao kila siku ya jumamosi
Vilevile, Mhe. Kaganda amewapongeza wananchi wote, watumishi na wadau waliojitokeza katika zoezi la Usafi wa mazingira.
Hata hiyo, Mhe. Kaganda amepata nafasi ya kuzungumza na wananchi na kuwaelimisha umuhimu wa kutunza mazingira.
Kauli Mbiu katika Maadhimisho ya Usafi wa Mazingira mwaka 2024 , "Urejeshwaji wa Ardhi iliyoharibiwa na Ustahimilivu wa hali ya Jangwa na Ukame"
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa