Mapema leo hii Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhandisi Richard Ruyango amemkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Wilaya ya Longido, ikiwa ni baada ya mbio za Mwenge wa Uhuru kukamilika kwa siku mbili katika Halmashauri mbili za Wilaya ya Arumeru ambapo miradi 18 yenye thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni 5 imetembelewa,imewekwa mawe ya msingi na kuzinduliwa.
Ikumbukwe Tarehe 23 Mbio za Mwenge wa Uhuru zilikimbizwa katika Halmashauri ya wilaya ya Arusha na tarehe 24 Juni 2022 katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Miradi yote 18 katika Wilaya ya Arumeru imeridhiwa na Mkimbiza Mwenge Kitaifa Bwana Sahili Nyanzabara Geraruma .
Arumeru Kazi iendelee
Kauli Mbiu ya Mbio za Mwenge Mwaka huu 2022
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa