Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mhandisi Richard Ruyango aagiza siku ya Jumanne kuwa siku ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi Wilayani humo
Ruyango amesema hayo katika Baraza la Halmashauri ya Wilaya Meru, ambapo amewataka Viongozi kuanzia ngazi za kitongoji, Vijiji, Kata na Wilaya kusikiliza na kutatua kero za wananchi "si vyema mwananchi anakero ambayo inaweza kutatuliwa na Viongozi wa eneo lake, atumie nauli na muda wake kuja ngazi za Wilaya" amehimiza Ruyango
Aidha katika kero ya Choo cha Soko la Usa -River Ruyango ametoa siku 30 Halmashauri kuhakikisha choo kinachengwa katika Soko hilo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Zainabu Makwinya baada ya kupokea maelekezo ya Mkuu wa Wilaya, amesema Choo Cha Soko la Usa-River kilifungwa kutokana na kujengwa karibu na mkondo wa maji, hivyo ameziagiza Idara na vitengo vyote kuhakikisha miradi yote ya Umma inatekelezwa baada ya kufanyika ukaguzi Ili kuongeza tija ya utekelezaji wa miradi hiyo "haiwezekani Serikali au wahisani kutoa fedha za mradi ambao baada ya muda mfupi unafungiwa" amehimiza Mwl.Makwinya
Vilevile Mwl.Makwinya amewataka Watumishi kusikiliza kero za wananchi kwa wakati sambamba na kutoa sababu za Msingi kwa kero ambazo zinazohitaji muda "waambieni Wananchi ukweli na mtoe sababu kwa kero zinazoitaji muda zaidi" ameagiza Makwinya.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mhandisi Richard Ruyango Akizungumza wakati wa Baraza la Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Mhe.Jeremia Kishilu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru,wakati wa Mkutano wa baraza la Halmashauri
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Zainabu Makwinya wakati wa Mkutano wa baraza la Madiwani.
Waheshimiwa Madiwani wakati wa Mkutano
Wakuu wa Idara na Vitengo wakati wa Mkutano wa baraza la Madiwani.
Waheshimiwa Madiwani wakati wa Mkutano
Wakuu wa Idara na Vitengo wakati wa Mkutano wa baraza la Madiwani.
Wakuu wa Idara na Vitengo wakati wa Mkutano wa baraza la Madiwani.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa