Halmashauri ya Meru na Arusha wagawana eneo.
Viongozi wa Halmashauri mbili za Meru na Arusha wilayani ya Arumeru, wafikiaa mufaka kugawana eneo lenye ukubwa wa mita za mraba 3200, lililoko eneo la Engira Road Jijini Arusha.
Awali eneo hilo lilikuwa likimilikiwa na iliyokuwa halmashauri ya Arumeru, ambayo ilivunjwa na 30Juni 2007 na tarehe 01 Julai, 2007 kuzaliwa halmashauri mbili za Arusha na Meru na kulazimika kugawana baadhi ya mali zilizokuwa zikimilikiwa na halmashauri hiyo ya Arumeru.
Makubaliano hayo yamefikiwa mara baada ya pande zote mbili, kukaa vikao vya kisheria katika halmashauri husika na hatimaye kukutana kwenye kikao cha pamoja, kilichosimamiwa na kuongozwa na Katibu Tawala wilaya ya Aruemru, Mwalimu James Mchembe, kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Arumeru.
Katika kikao hicho kilichojumuisha Waheshimiwa Madiwani wa Kamati ya Fedha Utawana na Mipango na timu ya Menejimenti ya halmashuri zote mbili za Arusha na Meru, na kufikia makubaliano ya kugawana eneo hilo nusu kwa nusu bila kujali majengo yaliyopo katika eneo hilo.
Aidha mgawanyo wa eneo hilo utawezesha halmashauri ya Arusha kupata mita za mraba 1,600, kadhalika halmashauri ya Meru kupata mita za mraba 1,600 pia.
Aidha baada ya makubaliano hayo, viongozi hao wamewaagiza watalamu wa Ardhi wa pande zote mbili kuanza mchakato wa kugawa eneo hilo kwa haraka na kupata hati miliki ya kila eneo, ili kila halmashauri iwe na hati miliki yake pamoja na kuanza kutumia maeneo hayo kwa manufaa ya wanachi wa halmashauri zote mbili.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa