Wanafunzi 96 katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru ambao ni miongoni mwa wanafunzi 1,635 wa kidato cha kwanza ambao hawakupangwa katika awamu ya kwanza kutokana na upungufu wa vyumba vya madarasa, wamepangwa katika Shule ya Sekondari Nkoarisambu baada vyumba viwili kukamilika.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Ndg.Emmanuel Mkongo amesema Halmashauri hiyo imeanza kuwapanga wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa awamu ya pili, ambapo leo wanafunzi 96 wamepangwa katika shule ya Sekondari Nkoarisambu hivyo kutimia kwa idadi ya wanafunzi 196 waliopangwa katika shule hiyo. Ameeleza kuwa kutokana na upungufu wa vyumba 2 vya madarasa wanafunzi 100 pekee walipangwa katika shule hiyo kwa awamu ya kwanza.
Mkongo amesema Halmashauri hiyo itaendelea kuwapanga wanafunzi wa awamu ya pili katika shule za Sekondari zitakazo kamilisha vyumba vya madarasa baada ya kufanya ukaguzi na kujiridhisha. Mkongo ameendelea kutoa wito kwa Waheshimiwa Madiwani ,Wenyeviti wa Vijiji, Wenyeviti wa Vitongoji, Watendaji wa Kata na Vijiji kusimamia ukamilishaji wa madarasa hayo kabla ya tarehe 28 Febriari 2021 kama Serikali ilivyoelekeza.
Aidha, ziara hiyo ya Ufuatiliaji na Ukaguzi wa ukamilishaji wa vyumba vya madarasa ilimjumuisha Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe. Jeremia Kishili, Mkurugenzi, Afisa elimu Sekondari na Mhandisi wa ujenzi. Shule za Sekondari zilizo tembelewa ni Ngongongare, Nkoarisambu na Shule mpya ya Sekondari Kiwawa inayotarajiwa kuanza wiki ijayo kwa kupangiwa wanafunzi , shule hii ni mpya ina vyumba vya 4 vya madarasa, viti na meza 100 kwaajili ya wanafunzi, imeelekezwa kukamilisha baadhi ya miundombinu ya maji kwa upande wa vyoo vya Ofisi ya Walimu kabla ya wiki ijayo.
Ikumbukwe, katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru idadi ya wanafunzi 6,851 walichaguliwa kujiunga kidato cha kwanza ambapo kati yao 5,216 walipangwa kwa awamu ya kwanza na 1,635 wanasubiri kupangwa kwa awamu ya pili baada ya vyumba vya madarasa kukamilika ambapo kati yao 96 wamepangwa leo.
Katika kuhakikisha vyumba vya madarasa vinakamilika Halmashauri ya Wilaya Meru kupitia fedha za mapato yake ya ndani (Own Source) imetumia zaidi ya Shilingi Milioni 160 kununua vifaa vya ujenzi ambavyo ni Bati 1860 zilizogharimu shilingi 48,259,004.51, Mbao shilingi 64,598,752.00 na Saruji mifuko 3325 iliyogharimu shilingi 48,212,500.
bofya hapa Kuona orodha ya wanafunzi 96 waliopangwa.pdf
Mkutugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ta Meru akiwa katika moja ya darasa katika Shule ya Sekondari Nkoarisambu.
Uongozi wakati wa Ziara katila shule ya Sekondari Kiwawa.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa