AWAMU YA SITA KAZINI, MILIONI 900 ZATOLEWA KWA AJILI YA UJENZI KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA MERU.
Imewekwa: March 4th, 2024
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Sita, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa sh. Milioni 900 za ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD), Maabara, kichomea taka cha kisasa pamoja na ukarabati wa majengo ya zamani katika Hospitali ya Wilaya ya Meru iliyopo Kata ya ya Akheri.
Akizungumza katika uzinduzi wa ujenzi wa mradi huo, Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Emmanuela Kaganda amesema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Meru imepokea fedha nyingi za utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na fedha sh. Milioni 900 zilizoelekezwa katika ujenzi wa jengo la OPD,Maabara,Kichomea taka na ukarabati wa majengo ya zamani katika Hospitali ya Wilaya ya Meru.
Mhe. Kaganda amezindua ujenzi wa mradi huo na kutoa maelekezo kwa kamati ya usimamizi wa mradi kuhakikisha wanasimamia ujenzi huo ili uweze kukamilika kwa wakati na kuleta manufaa kwa wananchi.
" Niwaombe kamati ya ujenzi kusimamia mradi huu na kuhakikisha taratibu zote zinafuatwa, lakini pia mafundi kufanya kazi hii kizalendo kwani hospitali hii inaenda kuhudumia ndungu zetu wananchi wengi ndani na nje ya Wilaya" alisema Kaganda.
Hata hivyo, Mhe. Kaganda amesisitiza utunzaji wa majengo yanayojengwa na Serikali ili yaweze kutumika kwa muda mrefu na manufaa ya vizazi vijavyo.
@ortamisemi