Mhe.Samia Suluhu Hassan,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mhe.Uhuru Kenyatta Rais wa Kenya ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wamewaongoza Wakuu wa Nchi nyingine za jumuia hiyo katika ufunguzi wa barabara ya mchepuo ya Jiji la Arusha (Arusha by pass) yenye urefu wa km 42.4 iliyogharibu Shilingi bilioni 197.4.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo ya ufunguzi katika viwanja TPRI Mringa Estate - Ngaramtoni
Mhe.Rais Samia amewashukuru Wakuu wa Nchi nyingine za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kuhudhuria hafla hiyo ya ufunguzi ambapo amesema barabara hiyo itachochea maendeleo kutokana na shughuli za kiuchumi zitakazokuwa zinafanyika ikiwa ni pamoja na utalii.
Vilevile Mhe.Rais Samia baada ya kutoa wito wa utunzaji wa miundombinu ya barabara hizo ametumia hafla hiyo kuwakumbusha Watanzania kushiriki Sensa ya Watu na Makazi itakayo fanyika tarehe 23 Agosti 2022 ikilenga kupata taarifa sahihi za kidemografia, kijamii, kiuchumi na hali ya mazingira kwa lengo la kupata takwimu sahihi zitakazoiwezesha Serikali na wadau wengine kupanga kwa usahihi mipango ya maendeleo.
Aidha, wilaya ya Arumeru imenufaika kupitiwa na barabara hii yenye urefu wa km 42.4 ya mchepuo ya jiji la Arusha (Arusha by pass) .
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa