Baraza la Wafanyakazi Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Wilayani Arumeru limepitia rasimu ya bajeti ya Halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha 2021/2022 yenye jumla ya shilingi bilion 46.3.
Mwenyekiti wa Baraza hilo Ndg.Emmanuel Mkongo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri, ametoa wito kwa watumishi kuongeza juhudi na ufanisi katika utendaji wao kwani jukumu kubwa la Halmashauri ni kutoa huduma kwa wananchi.
Mkongo ametaja changamoto zinazo athiri utoaji wa huduma ilkiwemo ulipaji wa stahiki mbalimbali za watumishi kwa wakati, kufanya kazi kwa mazoea na uwezo mdogo wa Halmashauri kujitegemea. Hivyo, ametoa wito kwa watumishi kuongeza juhudi, ufanisi na ubunifu katika kuongeza uwezo wa Halmashauri kujitegemea "uwezo wa Halmashauri hii kujitegemea ni asilimia 7 hivyo hatuna budi kuongeza juhudi na uwajibikaji kwa kutoa huduma bora na kubuni vyanzo vipya vya mapato kuongeza ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa vyanzo vilivyopo "amesisitiza Mkongo.
Mkongo amefafanua bajeti hiyo yenye jumla ya shilingi bilioni 46.3 inahusisha mapato ya ndani jumla ya shilingi bilioni 3.4, ruzuku ya mishahara Shilingi bilioni 35.7, ruzuku ya matumimizi mengineyo ni shilingi bilioni 1.7 na ruzuku ya miradi ya maendeleo ni shilingi bilioni 5.2.
Wakichangia kwa nyakati tofauti, watumishi wameiomba Serikali kuongeza umri wa ukomo wa watoto katika bima ya afya ya Taifa (NHIF) kutoka miaka 18 hadi 23 kwani jambo hilo ni kikwazo kikubwa kwao "mtumishi unawajibika kumlipia mtoto wako huduma za afya ambaye ana umri wa miaka chini ya 25 ambaye yupo Chuo Kikuu kwa kigezo cha umri kuzidi miaka 18" amesema Bi. Felister Lonjini
Aidha watumishi hao wameiomba Serikali kuwawezesha watumishi wanaojiendeleza kitaaluma kupanda madaraja na vyeo bila kuondoa miaka ambayo wameitumia masomoni sambamba na kuwajulisha watumishi sababu za kupanda au kutopanda vyeo.
Viongozi wa vyama vya wafanyakazi wameipongeza Halmashauri kughulikia maslai ya watumishi wastaafu na kutoa wito kwa Halnashauri kuwajengea watumishi uelewa wa maswala yanayogusa stahiki zao ambapo Katibu wa Chama cha wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya TUGHE (M), ndugu Samweli Magero ameomba Halmashauri kutoa elimu juu ya stahiki kwa Watumishi wanaojiendeleza.
Ikumbukwe rasimu ya bajeti hii ya Halmashauri ilipitishwa katika baraza la madiwani tarehe 10 februari 2021.
Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi Halmashauri ya Meru Ndg.Emmanuel Mkongo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri,kushoto ni Katibu wa baraza hilo Bi.Oliver Swatty.
Wakuu wa idara wakati wa mkutano baraza la wafanyakazi.
Mkuu wa idara ya utawala na rasilimali watu Bi. Grace Mbilinyi akitoa ufafanuzi wa maswala mbalimbali ya kiutumishi yaliohojiwa wakati wa baraza la wafanyakazi.
Katibu wa Chama cha wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya TUGHE (M), ndugu Samweli Magero akizungumza wakati wa Mkutano wa baraza la wafanyakazi Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Watumishi na viongozi wa watumishi wakati wa Mkutano wa baraza la wafanyakazi.
Watumishi na viongozi wa watumishi wakati wa Mkutano wa baraza la wafanyakazi.
Watumishi na viongozi wa watumishi wakati wa Mkutano wa baraza la wafanyakazi.
Watumishi wakati wa Mkutano wa baraza la wafanyakazi.
Watumishi wakati wa Mkutano wa baraza la wafanyakazi.
Watumishi wakati wa Mkutano wa baraza la wafanyakazi.
Watumishi wakati wa Mkutano wa baraza la wafanyakazi.
Bi. Angela Urasa ,Miongoni mwa watumishi waliotoa maoni
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa