Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mhe. Jeremia Kishili amewataka Waheshimiwa Madiwani na Watendaji wa Halmashauri na Kata kuendelea kutoa ushirikiano katika utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo ili kuweza kuisimamia miradi na kukamilika kwa wakati.
Mhe. Kishili amesema hayo katika Mkutano wa Baraza za Halmashauri la kujadili taarifa za Kata kwa kipindi cha mwezi Oktoba hadi Disemba 2023 kwa mwaka wa Fedha 2023/2024.