Halmashauri ya Wilaya ya Meru Leo Tarehe 31.08.2023 imefanya Mkutano wa Baraza la Halmashauri hiyo kwa kipindi cha robo ya nne Aprili hadi Juni kwa mwaka wa Fedha 2022/2023 ikiwa ni kuwasilisha taarifa kutoka katika Kata 26 zilizopo katika Halmashauri hiyo.
Waheshimiwa Madiwani wamewasilisha taarifa za utekelezaji za Kata kwa kipindi cha Aprili - Juni 2022/2023 na kueleza hali ya utoaji wa hudumu za kijamii kwa ujumla na utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo, Masuala ya Elimu katika Kata, hali ya shughuli za kiuchumi, mafanikio, changamoto na utatuzi wake, utunzaji wa mazingira na vyanzo vya maji pamoja na mipango ya baadae.
Utaratibu wa kuwasilisha taarifa za utekelezaji katika Mkutano wa Halmashauri ni kwa mujibu wa kanuni za kudumu za Halmashauri za mwaka 2014 chini ya kanuni ndogo ya 3(1).
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa