Wajumbe wa baraza la madiwani Halmashauri ya Meru, wilayani Arumeru, wamekubaliana kuwa na agenda ya kutokomeza mimba za utotoni na utoro shuleni kudumu kwenye vikao vya Vijiji na Kata kwa kujikita kuelimisha jamii kuanzia ngazi ya familia.
Wajumbe hao wameazimia hilo, mara baada ya, madiwani wa Kata kadhaa kuwasilishwa taarifa zinazoonesha changamo ya mimba za utotoni zinazowaka bili wanafunzi katika kata zao.
Awali taarifa hizo zimethibitishwa na Idara ya Elimu Msingi na Sekondari kuthibitisha kuwa jumla wanafunzi 67 wamepata mimba kwa mwaka 2017/2018.
Afisa elimu Sekondari Mwl Damari Mchome ameeleza kuwa kwa kipindi cha Mwezi Jan uari 2017 mpaka sasa jumla ya wanafunzi 57 waliripotiwa kupata mimba ambapo kati yao wanafunzi 27 wamepata mimba kuan zia mwezi Januari mwaka huu 2018.
Mwl.Mchome ametoa rai kwa wazazi kutekeleza jukumu la malezi kwa wanafunzi sambamba na kujenga mabweni ili kuwaepusha wanafunzi hao wa kike na vishawishi wanavyokutana navyo kwa kutembea umbali mrefu kwenda shule .
Nae mwakilishi wa Afisa elimu Msingi Mwl.Exaud Kimaro ameeleza kuwa kwa kipindi cha Mwezi Januari Mwaka 2017 hadi Mwezi Octoba mwaka huu jumla ya wanafunzi 10 wa shule za Msingi wamepata mimba na kushindwa kuendelea na Masomo.
Mwanasheria wa Halmashauri hiyo,wakili Magdalena John amesema Serikali iliweka sheria ili kumlinda Mwanafunzi kutokukosa fursa ya masomo ila changamoto kubwa katika kushughulika na kesi za mimba kwa wanafunzi ni utoaji wa ushahidi hivyo ametoa rai kwa wazazi na jamii kutoa ushahidi kwa wakati.
Makamu mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Nelson Mafie amesikitishwa na wazazi kutokua mstari wa mbele kutoa taarifa za wanafunzi kupata mimba na kusubiri viongozi kuja kuzitafuta. "tumeona hivi karibuni Mkuu wetu wa Wilaya Jerry Muro akipambana kutokomeza mimba kwa wanafunzi kwa kuwachukulia hatua wahusika , hivi wazazi na jamii tunakuwa tupo wapi ?' " Amehoji Mafie .
"Halmashauri imejipanga vipi kumaliza swala la mimba kwa wanafunzi ?"amehoji Diwani viti maalumu Kata ya Usa -River Meri Antony
Akihitimisha mjadala huo mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Will Njau, ametoa rai kwa viongozi wa dini ,mila na siasa kutoa elimu huku muongozo wa baraza hilo agenda ya kutokomeza mimba za utotoni kwa wanafunzi na utoro kuwa ya kudumu katika vikao ngazi za vijiji na kata .
Aidha Mkutano wa Baraza la Halmashauri ya Meru kwa kipindi cha Robo ya kwanza Julai -Septemba umekamilika kwa siku ya kwanza ambapo madiwani 3 toka Kata ya Kikwe,King'ori na Majengo walioshinda uchaguzi mdogo uliofanyika tarebe 13 Mwezi Octoba mwaka huu wameapishwa
Katikati ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Willy Njau ,kulia kwake ni Makamu Mwenyekiti Nelson Mafie na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji Emmanuel Mkongo.
Mwakilishi wa Afisa elimu Msingi ,Mwl.Exaud Kimaro akitoa taarifa yawanafunzi wa shule za msingi waliopata mimba
Afisa elimu Sekondari,Mwl.Damari Mchome akitoa taarifa yawanafunzi wa shule za sekondari waliopata mimba.
Mwanasheria wa Halmashauri ya Meru ,wakili Magdalena John akitoa ushauri wa kisheria katika baraza la Halmashauri.
Mhe. Diwani Kata ya Imbaseni Gadiel Mwanda akiwasilisha taarifa ya kata hiyo katika baraza la Halmashauri.
Mhe.Elisa Mungure Diwani Kata ya Kikatiti akiwasilisha taarifa ya kata hiyo katika baraza la Halmashauri.
Mhe. Peter Kessy Diwani Kata ya King'ori akiwasilisha taarifa ya kata hiyo katika baraza la Halmashauri.
Mhe.Anderson Sikawa Diwani Kata ya Leguruki akiwasilisha taarifa ya kata hiyo katika baraza la Halmashauri.
Mhe.Bernad Kivondo Diwani Kata ya Majengo akiwasilisha taarifa ya kata hiyo katika baraza la Halmashauri.
Mhe. Diwani Kata ya Makiba Samson Laizer akiwasilisha taarifa ya kata hiyo katika baraza la Halmashauri.
Mhe.Diwani Kata ya Ngarenanyuki Zakaria Nnko akiwasilisha taarifa ya kata hiyo katika baraza la Halmashauri.
Mhe.Charles NnkoDiwani Kata ya Songoro akiwasilisha taarifa ya kata hiyo katika baraza la Halmashauri.
Waheshimiwa Madiwani wakisikiliza taarifa za wanafunzi waliopata Mimba.
Waheshimiwa Madiwani wakisikiliza taarifa za wanafunzi waliopata Mimba.
Waheshimiwa Madiwani wakisikiliza taarifa za wanafunzi waliopata Mimba.
Waheshimiwa Madiwani wakisikiliza taarifa za wanafunzi waliopata Mimba.
Waheshimiwa Madiwani wakisikiliza taarifa za wanafunzi waliopata Mimba.
Wakuu wa idara na vitengo wakisikiliza taarifa za wanafunzi waliopata Mimba.
Wakuu wa idara na vitengo na wananchi wakisikiliza taarifa za wanafunzi waliopata Mimba.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa