Halmashauri ya Wilaya ya Meru imefanya Mkutano wa Baraza la Halmashauri kwa siku ya Pili lililotanguliwa na maswali ya Papo kwa Papo kwa Mheshimiwa Mwenyekiti wa Halmashauri na Mkurugenzi Mtendaji.
Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Halmashauri Leo Tarehe 03.10.2023.
Kwa Mujibu wa Kanuni ya 24 ya kanuni za kudumu za Halmashauri ya Wilaya ya Meru za mwaka 2014, wajumbe wamepata nafasi ya kuuliza maswali ya Papo kwa Papo kwa Mheshimiwa Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri.
Aidha, Wenyeviti wa Kamati za kudumu za Halmashauri wamewasilisha taarifa za Kamati zao na kutolea ufananuzi kwenye maeneo ambayo yamehitaji ufafanuzi.
Ambapo, moja ya Masuala yaliyojadiliwa na kutolewa maelekezo ni pamoja na suala la uwiano wa walimu na wanafunzi katika shule za Msingi zilizopo Wilayani humo.
Kamati hizo ni Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango, Kamati ya Elimu, Afya na Maji, Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira pamoja na Kamati ya Mpango wa kudhibiti UKIMWI.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Jeremia Kishili ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuleta Fedha nyingi za utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo.
Vilevile, Katibu wa Mkutano huo Mkurugenzi Mtendajiwa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl. Zainabu J. Makwinya ametoa tahadhari ya Mvua kubwa za El nino na kusisitiza kuwa mvua hizi zinazoendelea kunyesha zitumike kulima na kupanda mazao yanayoendana na Mvua kwani Utabiri wa Hali ya hewa uliotolewa na mamlaka ya Hali ya hewa wameeleza kuwa mvua hizi zinaweza kunyesha hadi mwezi Januari 2024.
Pia Mwl. Zainabu amekumbushia maandalizi ya Bajeti kwa ngazi ya chini kufanyika mapema na kuchagua miradi yenye tija na itakayo malizika na siyo kupanga miradi mingi ambayo haitaweza kukamika na kuacha viporo.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa