Halmashauri ya Wilaya ya Meru Leo Tarehe 01.09.2023 imefanya Mkutano wa Baraza la Halmashauri kwa siku ya Pili.
Kwa Mujibu wa Kanuni ya 24 ya kanuni za kudumu za Halmashauri ya Wilaya ya Meru za mwaka 2014, wajumbe wamepata nafasi ya kuuliza maswali ya Papo kwa Papo kwa Mheshimiwa Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri.
Aidha, Wenyeviti wa Kamati za kudumu za Halmashauri wamewasilisha taarifa za Kamati zao na kutolea ufananuzi kwenye maeneo ambayo yamehitaji ufafanuzi.
Kamati hizo ni Kamati ya Fedha,Utawala na Mipango, Kamati ya Elimu, Afya na Maji, Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira pamoja na Kamati ya Mpango wa kudhibiti UKIMWI.
Vilevile, Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe.Jeremia Kishili amewashukuru wajumbe wote kwa ushirikiano waliompa kwa kipindi chote cha mwaka wa Fedha 2022/2023 na amewatakia kila la Kheri wajumbe wote katika kuanza kutekeleza shughuli mbalimbali kwa mwaka mpya wa Serikali wa 2023/2024.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa