• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Meru District Council
Meru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Meru

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, Takwimu na Ufatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Utumishi na Utawala
      • Usafi na mazingira
      • Ardhi na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Manunuzi na ugavi
      • Uchaguzi
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Misitu
    • Ufugaji wa Ngombe wa Maziwa
    • Ujenzi wa Kituo cha Biashara
    • Ujenzi wa Eneo la Mapumziko
    • Ujenzi wa kituo cha Mabasi cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Malori cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Michezo
    • Kilimo cha Nyanya
    • Ufugaji wa Nyuki
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • AIDS
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Miongozo
    • Fomu mbalimbali
    • Utaratibu
  • Kituo cha habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

BARAZA LA MADIWANI HALMASHAURI YA MERU LAIDHINISHA BAJETI BILIONI 54.1, MWAKA WA FEDHA 2023/2024

Imewekwa: February 21st, 2023

Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru laidhinisha rasimu ya bajeti  ya mwaka wa fedha 2023/2024  kiasi cha Bilioni 54.1 ambapo kati ya fedha hizo kiasi cha Bilioni 5.31 ni  mapato ya ndani ya Halmashauri.

Akizungumza wakati wa mkutano maalum wa baraza hilo,Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Mhe.Jeremia Kishili amesema rasimu hiyo  ya bajeti kiasi cha Bilioni 54.1 imejikita kuwaletea wanananchi maendeleo ikiwa ni kuongeza na kuboresha miundombinu ya huduma za kijamii, ambapo katika rasimu hiyo kiasi cha bilioni 10.49 kimetengwa kama fedha za maendeleo kwa mchanganuo wa bilioni 1.3 ni fedha za maendeleo zitokanazo na mapato ya ndani na bilioni 9.19 ni fedha za maendeleo toka Serikali Kuu.

Vilevile, Mhe.kishili  amebainisha Halmashauri hiyo kuendelea  kukusanya mapato na kuwaletea wananchi maendeleo sambamba na kuhakikisha fedha zote zinazoletwa kwa ajili ya shughuli za maendeleo zinasimamiwa ipasavyo ili kuleta tija iliyokusudiwa ambapo amewataka  wakusanya mapato ya Halmashauri kuwa waadilifu na ufanisi Mkubwa. Pia ametoa wito kwa wananchi kudai  risiti kwa malipo ya tozo za Halmashauri .

Awali, akiwasilisha rasimu hiyo  kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Bw.Daudi Wengi, Afisa Mipango  Halmashauri  hiyo ameeleza katika rasimu hiyo ya bajeti  kiasi cha Bilioni 54.1, kiasi cha Bilioni  5.3 ni fedha zitokazano na vyanzo vya mapato ya ndani, kiasi cha bilioni 38.41 ni ruzuku ya mishahara, kiasi cha bilioni 1.18 ni ruzuku ya matumizi mengine na kiasi cha bilioni  9.19 ni fedha za maendeleo ya ndani na nje.

Ikumbukwe, Mpango huo wa bajeti umeandaliwa kwa mujibu wa kifungu Na. 11 cha  sheria ya Sheria ya Bajeti Na. 21 ya mwaka 2015 pamoja na Kanuni zake, maelekezo na mwongozo wa kitaifa maandalizi ya Bajeti, unaoelekeza  kupokea mapendekezo na vipaumbele kisekta kuanzia ngazi ya vitongoji, vijiji, kata, Idara na Vitengo vya halmashauri.

Meru Dc tupo vizuri






Matangazo ya Kawaida

  • KUITWA KWENYE USAILI ANWANI ZA MAKAZI April 02, 2022
  • waliochaguliwa kwenye usaili wa tarehe 5 Aprili 2022 April 07, 2022
  • TANGAZO LA AJIRA NAFASI YA KAZI KATIBU MAHSUSI DARAJA 111 May 26, 2022
  • MILIONI 50 ZA TOZO ZAKAMILISHA VYUMBA VINNE VYA MADARASA September 22, 2022
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • WASIOKAMILISHA MALIPO KUNYANG'ANYWA VIWANJA/MASHAMBA

    March 01, 2023
  • MHE.RAIS KUWASALIMIA WANANCHI WA ARUMERU

    March 04, 2023
  • BARAZA LA MADIWANI HALMASHAURI YA MERU LAIDHINISHA BAJETI BILIONI 54.1, MWAKA WA FEDHA 2023/2024

    February 21, 2023
  • Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru akabidhi Ofisi

    February 01, 2023
  • Tazama Vyote

Video

Salamu za sikukuu ya Krismasi na Mwaka mpya 2021.
Video Zaidi

Viungo Haraka

  • Kupata Salary Slip
  • Sheria ndogo za Halmashauri ya Wilaya ya Meru

Kiungo Kuhusiana

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Utumishi
  • Watumishi Portal
  • Tovuti ya Mkoa wa Arusha
  • Ajira Portal
  • Government Salary Slip Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Meru

    Anwani: P.o. Box 462 Usa River

    Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@merudc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa