Ujenzi wa Kituocha Afya cha kisasa chenye thamani ya Milioni 400 kutekelezwa kupitia Bajeti ya Halmashauri ya Wilaya ya Meru yenye jumla ya shilingi 46,375,641,181.10 iliyopitishwa na Baraza la Halmashauri hiyo kwa mwaka wa Fedha 2021/22 .
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Jeremiah Kishili amesema madiwani wamepitisha bajeti hiyo yenye jumla ya shilingi 46.3 ambapo mchanganuo wake ni mapato ya ndani shilingi bilioni 3.4, mishahara shilingi bilioni 35.7, ruzuku ya matumimizi mengineyo shilingi bilioni 1.7 na ruzuku ya miradi ya maendeleo ni shilingi bilioni 5.2.
Naye , Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Ndg.Emmanuel Mkongo amesema katika bajeti ya mapato ya ndani ya shilingi bilioni 3.4, Halmashauri hiyo imeelekezwa na Serikali kuboresha huduma za afya kupitia mapato yake ya ndani ambapo jumla ya shilingi Milioni 400 zimetengwa kwaajili ya ujenzi wa Kituocha Afya katika mwaka wa fedha 2021/2020 .
Mkongo amesema maelekezo hayo yalitolewa siku chache kabla ya Mkutano huo ambapo Waheshimiwa Madiwani wamependekeza Kituocha Afya kujengwa katika Kata ya Maroroni.
Mkongo ametoa wito kwa Madiwani kushikiana kikamilifu na Watumishi katika kukusanya mapato ili kuweza kuwaletea wananchi maendeleo “ili kukamilisha kituo hicho cha afya chenye thamani ya shilingi milioni 400 ambazo ni fedha za makusanyo ya mapato ya ndani hatuna budi kukusanya mapato kwa asilimia 100%” amesisitiza Mkongo.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo, Dkt.Maneno Focus amesema Halmashauri ina vituo vya afya 10 ambapo kati ya hivyo saba ni vya Serikali ambapo katika Tarafa ya king'ori kuna vituo vitatu, Tarafa ya Poli vinne na Tarafa ya Mbuguni vinne.
Dkt.Focus ameeleza zaidi kuwa Halmashauri hiyo ina upungufu wa vituo vya afya katika kata 18 sawa na asilimia 69 ambapo ujenzi wa kituo hicho utapunguza changamoto za Mama na Mtoto na kuondoa changamoto ya umbali kwa wananchi kupata huduma.
Mhe.Diwani wa Kata ya Maroroni Yona Kaaya amesema ujenzi wa kituo hicho cha afya utakwenda kutatua changamoto walizokuwa wanakumbana nazo wananchi ikiwemo umbali mrefu, mrundukano wa watu katika baadhi ya vituo vya afya.
Ikumbukwe kuwa katika Mwaka wa fedha 2017/18, Serikali iitoa Shilingi Milioni 500 kwaajili ya ujenzi na uboreshaji wa Kituo cha Afya Usa- River katika Halmashauri ya Wilaya ya MERU ambacho kimeboresha upatikanaji wa Huduma bora za afya.
BAADHI YA PICHA .
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Ndg.Emmanuel Mkongo akizungumza wakati wakikao.(kushoto)ni Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe.Jeremia Kishili.
Waheshimiwa Madiwani wakati wa kikao.
Waheshimiwa Madiwani wakati wa kikao.
Waheshimiwa Madiwani wakati wa kikao.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa