Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Wilayani Arumeru inatarajia kutengeneza meza Mia sita kwa ajili ya wafanyabiashara wa soko la Tengeru ikiwa ni mikakati ya uboreshaji wa miundombinu ya masoko na uwekaji mazingira rafiki ya kibiashara na kuimarisha vyanzo vya mapato.
Akizungumza wakati wa Mkutano wa baraza la Halmashauri hiyo Mhe.Julius Mungure Diwani wa Kata ya Akheri amepongeza hatua zinazoendelea za uboreshaji wa Soko la tengeru ambapo mbali na Halmashauri kufanya ukarabati mdogo wa miundombinu katika choo cha soko hilo inaendelea na mchakato wa kutengeneza Meza 600 kwa ajili ya wafanyabishara.
Mhe.Mungure amesema utengenezaji huo wa meza Mia sita unatija kubwa kwani utaondoa adha waliyokuwa wanapata wananchi ya kupanga bidhaa chini ambapo ameshauri meza zilizopo katika soko hilo kuboreshwa ili ziendelee kutumika.
Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Zainabu Makwinya amesema Halmashauri itatengeneza Meza mia sita kwa ajili ya wafanya biashara wa soko la Tengeru ili kuongeza idadi ya meza katika soko hilo kwani huko nyuma Halmashauri ilishatengeneza meza 200 na baadhi zinaitaji ukarabati.
Vilevile Mwl.Makwinya amesema uboreshaji huo ni pamoja ukarabati mdogo wa miundombinu ya choo cha soko hilo, ambao umekua nne ya kiasi kilichokuwa kikikusanywa awali cha Shilingi laki moja na elfu ishirini kwa mwezi.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mhe. Jeremia Kishili amesema wakati uboreshaji huo unaendelea ni muhimu kwa wafanyabiashara kufanya biashara kwa usalama kwa kuondoka maeneo ya barabarani na kuingia ndani ya soko.
Mkutano wa Baraza la Halmashauri wa siku mbili umehitimishwa katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa