Wajumbe wa Kamati ya kusimamia viongozi Wakuu wa Kitaifa , Baraza la Uwakilishi la Zanzibar wamepongeza utekelezaji wa Miradi ya TASAF OPEC III katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru ,Wilayani Arumeru na kutoa wito kwa jamii kutumia vizuri miradi hiyo ikiwa ni kuitunza ili idumu na kuleta tija iliyokusudiwa.
Wajumbe hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe.Machano Othman Said, wameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendeleza mpango wa TASAF OPEC III unaolenga kumkwamua Mwananchi kuondokana na umaskini
Machano amesema Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan anahakikisha Watanzanua wote wanapata maendeleo ambapo utekelezaji wa Mradi wa TASAF OPEC III na miradi mingine kwa ujumla ni jitihada za kudumisha Umoja, amAmani na Mshikamano kwa kuwaletea watanzania maendeleo " watumishi wa zahanati ya Kandashe wametoka mikoa mbalimbali kuja kuwahudumia na kupitia TASAF wamepata nyumba ya kuishi hivyo miradi imeendeleza umoja wetu sisi Watanzania"amesema
Naye Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo, Mtumwa yusuph ambaye ni mwakilishi wa jimbo la bubwini ametoa wito kwa jamii kutimiza wajibu wao katika malezi sambamba na kuitunza Miradi hiyo ya TASAF kuifanyia usafi ,kukarabati kwa wakati ili kuepusha madhara makubwa sambamba na kuwapa ushirikiano watumishi wanaopangwa kufanya kazi kwenye miradi hiyo " niwasihi wazazi tutekeleze jukumu letu watoto waende shule na tuhakikishe tunahusika katika malezi ya watoto kwani kizazi cha leo ndio tunachokitegemea kwa kesho" amesema
ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara yao katika Halmashauri ya Meru wametembelea miradi ya Ujenzi wa Vyumba vinne vya madarasa shule ya msingi Noseiya, Ujenzi wa Zahanati ya Kandashe pamoja na ujenzi wa Nyumba ya Mtumishi zahanati ya Kandashe.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe.Emmanuela Kaganda amepongeza miradi ya TASAF kufanyika vizuri
Wakizungumza kwa nyakati tofauti Wananchi wa Kijiji cha Kandashe wamesema miradi hiyo ya TASAF ni mkombozi kwao kwani kupitia Zahanati ya Kandashe kwa sasa wanapata huduma za matibabu masaa 24.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa