Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Ndg.Charles Kabeho alipoweka jiwe la msingi kwenye mradi wa maji kijiji cha Nshupu Halmashauri ya Wilaya ya Meru ,ameitaka kamati ya maji ya Kijiji hicho kupanga bei ya maji kwa kuzingatia hali ya kiuchumi wa wananchi .
Ndg.Kabeho amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji katika umbali usiozidi mita 400 hivyo uwepo wa miradi ya maji karibu na wananchi lazima uendane na gharama za kupata maji kwa kwa kuzingatia hali ya kiuchumi ya wananchi.
Aidha Ndg.Kabeho ametoa wito kwa katibu mkuu wizara ya maji kupeleka fedha zinazoitajika kukamilisha miradi ya Maji katika Halmashauri hiyo ya Meru kwani miongoni mwa miradi inayohitaji fedha hizo ili kukamilika ni mradi huo wa maji Kijiji cha Nshupu.
PICHA ZA TUKIO.
Mhandisi wa Halmashauri ya Meru ,Eng Happyness Mrisho akisoma taarifa ya Mradi wa Maji Kijiji cha Nshupu.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa akizungumza kabla ya kuweka jiwe la msingi katika Mradi wa Maji kijiji cha Nshupu.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Ndg.Charles Kabeho akiweka jiwe la msingi katika Mradi wa Maji kijiji cha Nshupu.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa akimkabidhi mwenyekiti wa kamati ya maji kijiji cha Nshupu, Joseph Kiware cheti cha makabidhiano ya mradi na katiba ya kuendesha mradi huo wa maji kijiji cha Nshupu baada ya kuweka jiwe la msingi katika Mradi wa Maji kijiji cha Nshupu.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa