Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Idd Kimanta,amepongeza juhudi za ukamilishaji wa vyumba vya madarasa katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru Wilayani Arumeru.
Hayo yamejiri wakati wa ziara yake ya siku mbili katika Wilaya ya Arumeru ambapo kwa siku ya kwanza imeanza katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru na siku ya pili itakuwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Arusha.
Akisoma taarifa mbele ya Mkuu huyo wa Mkoa, Mkuu wa Shule ya Sekondari Patandi Maalum Mwl.Janeth Mollel amesema mbali na Serikali kutumia zaidi ya Bilioni 3.4 kwaajili ya ujenzi wa miundombinu ya shule hiyo ya mfano nchini bado kunauhitaji wa ukamilishaji wa miundombinu muhimu na rafiki yenye thamani ya shilingi milioni 800 ili kuwezesha kuwapokea wanafunzi 185 wa kidato cha kwanza waliopangwa shuleni hapo.
Mwl.Molel amechanganua kuwa kati ya Wanafunzi 185 wanafunzi 136 ambapo wavulana ni 66 na wasichana ni 70 ni wanafunzi wenye mahitaji maalum wa bweni nMheshimiwa Idd Kimanta,na wanafunzi 49 waliobaki ni wa kutwa.
Mwl. Mollel amesema miundombinu iliyokamilika shuleni hapo ni mabweni manne ,mawili ya wasichana na mawili ya wavulana , madarasa 12 ya kidato cha kwanza hadi kidato cha nne, kwa utaratibu wa madarasa 3 kwa kila kidato kwa wastani wa wanafunzi 47.
Aidha. Mwl. Mollel amesisitiza kuwa kwa kuzingatia wanafunzi 136 waliopangwa ni wenye mahitaji maalumu kuna haja ya kutatua changamoto ya mahitaji muhimu ambayo mi vitanda double deka 10, magodoro 20, viti na meza 80 kwaajili ya matumizi ya wanafunzi darasani pamoja na ujenzi wa maabara ya sayansi, kuongeza mfumo wa maji taka, kuchimba kisima cha maji na mfumo wa kusambaza maji, kujenga mfumo wa jiko la gesi na jiko la tahadhari la kuni na ujenzi wa nyumba tatu kwa ajili ya Mwalimu, Patroni na Matroni pamoja na kuajiri Watumishi muhimu kwa Wanafunzi wenye mahitaji maalum.
Naye Ndg.Emmanuel Mkongo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya MERU amesema katika kutatua changamoto hizo Halmashauri hiyo imefanya juhudi za kuomba fedha za mahitaji muhimu katika Ofisi ya Rais TAMISEMI. Aidha, kutokana na changamoto za ukosefu wa miundombinu hiyo na kusubiri kupokelewa kwa fedha za ujenzi, Halmashauri imeandika barua Ofisi ya Rais TAMISEMI kuomba muongozo wa kusogeza muda wa kuwapokea wanafunzi hao kwa miezi mitatu (3) ili kukamilisha miundombinu hiyo ikiwemo uchimbaji wa kisima na miundombinu ya maji safi na salama, mfumoza wa maji taka ,
jenereta,ujenzi wa kuchomea taka,nyumba za kuishi mwalimu mkuu sambamba na mahitaji ya rasilimali watu, "wanafunzi hawa wenye uhitaji maalumu wanahitaji mazingira bora na wezeshi "amesisitiza Mkongo.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Ndg.Jerry Muro amesema Serikali imewekeza sana katika shule hiyo lakini hadi sasa bado wanasubiri mwongozo kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI kwani fedha zaidi ya shilingi milioni 800 zinahitajika kukamilisha miundombini rafiki kwa wanafunzi shuleni hapo.
Akihitimisha ziara yake katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru , Mkuu wa Mkoa wa Arusha amesitisha kuanza rasmi kwa shule hiyo tarehe 11 mwezi huu na kuahidi kutafuta ufumbuzi mapema ili wanafunzi hao waweze kuanza masomo yao.
Aidha, Mkuu wa Mkoa ametembelea na kukagua Vyumba vya Madarasa katika Shule za Sekondari za Akheri, Patandi Maalum, Nshupu, Sing'si, Kikwe na Muungano pamoja na Shule mpya ya Msingi ya Faye Crene Chem Chem iliyojengwa kwa ufadhili wa Rotary Club.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa