Shirika la Taifa la Bima ( NIC) kupitia Afisa Bima kanda ya Kaskazini Alfred Bwojo akimuwakilisha Meneja wakanda, wamefika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Meru kuomba ushirikiano juu ya kampeni watakayo iendesha ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Meru, kampeni ijulikanayo Kwa jina la BIMA MTAA KWA MTAA yenye Lengo lakusaidia watanzania wengi kuwa na Bima, ikijumuisha Bima ya Jengo, Bima ya Moto, Bima ya Gari n.k. Aidha Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl. Zainabu Makwinya ameahidi kutoa ushirikiano wa hali ya Juu kama walivyohitaji nakuwataka seemu yoyote watakayokwama wasisite kumjulisha.Aidha NIC wamempatia Mkurugenzi Mtendaji na Afisa usafirishaji Meru DC zawadi kama ishara ya kumbukumbu wakazi watakayo kwenda kuitekeleza
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa