Viongozi mbalimbali na Watumishi kutoka katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru wameshiriki katika ufunguzi wa Kongamano la Nne la Taasisi za Ardhi Afrika lenye ajenda ya " Upatikanaji wa Hatimiliki za Ardhi".
Kongamano hilo limefunguliwa leo na Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri wa Nishati kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan lililofanyika katika Hotel ya Mount Meru Mjini Arusha.
Imeelezwa kuwa kongamano Hilo limehusisha washiriki zaidi ya 100 kutoka takribani nchi 20 za Afrika na nje ya Afrika.
Dr. Biteko akiwasili katika Hotel ya Mountmeru iliyoko Arusha tayari kwa ufunguzi wa Kongamano la nne la Taasisi za Ardhi Afrika
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa