Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Eng.Richard Ruyango ametoa wito kwa Viongozi wa jamii, madhehebu ya dini kuelimisha Umma juu ya huduma za chanjo ya UVIKO - 19 ikiwa fursa kwa wananchi ambao wapo tayari kuchanjwa na kupunguza athari za kupata ugonjwa na madhara makubwa.
Eng.Ruyango ametoa Wito huo wakati wa uzinduzi wa chanjo ya UVIKO - 19 katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru ambao umefanyika katika Kituo cha Afya chw Usa-River .
Aidha,Ruyango amewataka Wananchi kuchukua tahadhari ya ugonjwa huu ambapo amepiga marufuku mikusanyiko kwenye misiba pia ametoa wito kwa Viongozi wa Dini kufupisha Ibada na kuwakumbusha waumini kuchukua tahadhari.
Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo Dkt.Maneno Focus amesema chanjo ya UVIKO -19 ni afua nyingine katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Uviko 19 ambapo walengwa 5410 wanatarajiwa kupata chanjo katika awamu ya kwanza ambapo ameanisha makundi yatakayoanza kupata chanjo ni pamoja na watumishi wa afya,walimu,vyombo vya ulinzi na usalama ,wenye magonjwa Sugu na wazee.
Nao Wanachi ambao wamepata fursa ya kupata chanjo ya UVIKO - 19 wameishukuru Serikali kwa kuleta chanjo hiyo na kuiomba mbali na kuchanjwa makundi yaliyoainishwa iendelee kupanua wigo wa utoaji chanjo hiyo kwa makundi mengine.
Aidha, Katika uzinduzi huo Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mheshimiwa Eng.Richard Ruyango amekuwa wa kwanza kupata chanjo hiyo akifuatiwa na Aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Ndg.Emmanuel John Mkongo ambaye amehamishiwa katika Halmashauri ya Mji wa Bunda, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo, Viongozi wa Dini akiwemo Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Meru, Paroko wa Parokia ya USA RIVER, Viongozi wa vyama vya Siasa ,Waheshimiwa Madiwani na wawakilishi wa watu wenye ulemavu.
Zoezi hilo linatarajiwa kuendelea katika vituo vya Hospitali ya Wilaya ya Meru na Kituo cha Afya Usa River.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Eng.Richard Ruyango wakati wa chanjo ya UVIKO - 19
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Eng.Richard Ruyango akichanjwa chanjo ya UVIKO - 19.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Eng.Richard Ruyango akiwa na Cheti baada ya kuchanjwa chanjo ya UVIKO - 19.
Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo Dkt.Maneno Focus akichanjwa chanjo ya UVIKO - 19
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Ndg.Emmanuel John Mkongo akipigwa chanjo ya UVIKO -19
mwenyekiti wa kamati ya Elimu afya na maji Halmashauri ya Meru,Diwani wa Kata ya Songoro akipata chanjo ya UVIKO-19
Mkuu wa TAKUKURU Wilaya ya Arumeru Ngd.Deo Mtui akipata Chanjo ya UVIKO -19.
Askofu wa KKKT Dayosisi ya Meru Elias Kitoi Nassari wakati wa Chanjo ya UVIKO -19.
Askofu wa KKKT Dayosisi ya Meru Elias Kitoi Nassari wakati wa Chanjo ya UVIKO -19
Askofu Issangya wa Sakila International Evangilism akiwa na Cheri baada ya kupata chanjo ya UVIKO -19.
Mhe.Diwani wa Kata ya USA - River baada ya kupata chanjo ya UVIKO -19
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa