• Barua pepe |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
Meru District Council
Meru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Meru

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, Takwimu na Ufatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Utumishi na Utawala
      • Usafi na mazingira
      • Ardhi na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Manunuzi na ugavi
      • Uchaguzi
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Misitu
    • Ufugaji wa Ngombe wa Maziwa
    • Ujenzi wa Kituo cha Biashara
    • Ujenzi wa Eneo la Mapumziko
    • Ujenzi wa kituo cha Mabasi cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Malori cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Michezo
    • Kilimo cha Nyanya
    • Ufugaji wa Nyuki
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • AIDS
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Miongozo
    • Fomu mbalimbali
    • Utaratibu
  • Kituo cha habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

CHANJO YA POLIO AWAMU YA TATU YAZINDULIWA RASMI WATOTO ZAIDI ELFU 56 KUCHANJWA.

Imewekwa: September 1st, 2022

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mhandisi Richard Ruyango amezindua rasmi kampeni ya awamu ya tatu ya chanjo ya  Polio itakayofanyika kwa Siku nne kuanzia leo tarehe 01 hadi 4 Septemba 2022, ambapo  ametoa wito kwa  jamii  kuwalinda watoto dhidi ya ugonjwa Polio unaosababisha  kupooza na  ulemavu wa viungo, kwa kuhakikisha watoto wote wenye umri chini ya miaka mitano  wanapata chanjo.

Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika katika hospitali ya Wilaya ya Meru (tengeru) Mhe. Ruyango  amesema  baada ya kugundulika uwepo wa ugonjwa huo nchi ya jirani ya Malawi  Serikali ya awamu ya  Sita chini ya Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan imehakikisha chanjo zinapatikana na watoto wanakuwa salama" chanjo ya Polio ni bure ni wasihi tuwalinde watoto kwa kuwapa chanjo"amehimiza Mhe.Ruyango

Dkt.Focus Maneno ambaye ni Mkuu wa Idara ya huduma za Afya, Lishe na ustawi wa jamii amesema ugonjwa wa polio hauna tiba na  ni hatari kwani unasababisha mtoto kupooza hivyo kupata ulemavu wa viungo  na kusababisha mtoto kuwa tegemezi ambapo amehimiza wazazi na walezi kuzuia madhara ya Polio kwa kuhakikisha watoto wanapata chanjo " mtoto asiyepata chanjo ni hatari kwake na kwa jamii nzima" amehimiza Dkt.Maneno.

Naye Mratibu wa chanjo Halmashauri ya Wilaya ya Meru Salome Mbegela amesema chanjo ya polio itatolewa kwa siku nne kuanzia leo tarehe 1 hadi 4 Septemba 2022 na itatolewa nyumba kwa nyumba, vituo vya huduma za afya, vituo vya kulelea watoto, katika shule  nk

Bryson Willium ambaye ni mzazi mwenye mtoto aliyepata chanjo ametoa wito kwa wazazi wote kushiriki kuwapa watoto chanjo ya Polio kwani ugonjwa huo ni hatari " nitoe wito kwa kina baba  wote kuwa mstari wa mbele kuwasaidia watoto kupata chanjo ya Polio kwani ni wajibu wa kila mzazi (baba na mama )na jamii yote kuwalinda watoto dhidi ya magonjwa ikiwa ni pamoja na Polio" amesema Bryason

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mhe.Jeremia Kishili ametoa wito kwa jamii kushiriki zoezi la chanjo ya Polio kuzuia  ulemavu wa viungo unaosababisha kupooza kutokana na ugonjwa wa polio

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Zainabu Makwiya ametoa wito kwa jamii kuhimizana ili watoto wote wenye umri chini ya miaka 5 wapate chanjo hiyo.

Ikumbukwe Halmashauri ya Wilaya ya Meru inatarajia kutoa chanjo ya Matone ya Polio kwa watoto elfu 56,591

Matangazo ya Kawaida

  • KUITWA KWENYE USAILI October 28, 2024
  • KUITWA KWENYE USAILI June 24, 2024
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MTAALA WA ELIMU YA AWALI NA MSINGI 2022. February 18, 2022
  • UUZAJI WA VIWANJA ENEO LA NGURUDOTO LIMEANZA. November 27, 2018
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • AJIRA MPYA MERU DC WAPATIWA MAFUNZO

    April 02, 2025
  • NAIBU WAZIRI MAENDELEO YA JAMII,JINSIA WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUMU AKAGUA MIRADI YA S.O.S

    March 15, 2025
  • MAFUNZO YA MFUMO WA TAUSI MERU DC YAFUNGWA

    February 15, 2025
  • TAHAPAO NA MERU DC WAWEKA NGUVU KWENYE KAMATI ZA MTAKUWA

    February 19, 2025
  • Tazama Vyote

Video

ELIMU YA KUKABILIANA NA TAHADHARI YA MVUA ZA EL NINO YAANZA KUTOLEWA HALMASHAURI YA MERU.
Video Zaidi

Viungo Haraka

  • Kupata Salary Slip
  • Sheria ndogo za Halmashauri ya Wilaya ya Meru

Kiungo Kuhusiana

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Utumishi
  • Watumishi Portal
  • Tovuti ya Mkoa wa Arusha
  • Ajira Portal
  • Government Salary Slip Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Meru

    Anwani: P.o. Box 462 Usa River

    Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@merudc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa