Mkuu wa Wilaya ya Arumeru mhandishi Richard Ruyango ameiagiza TARURA kuona namna ya kushirikiana na Halmashauri ya Meru kutengeneza barabara ya Usa-River inayoelekea eneo la makaburini, ikiwa ni utatuzi wa changamoto inayowakabili Wananchi wakati wa kuwapunzisha wapendwa wao kutokana na barabara hiyo kutokupitika haswa kipindi cha mvua "Serikali imeongeza bajeti ya TARURA Mara tatu zaidi, kutoka Milioni 500. hadi Bilioni 2. hivyo ni wajibu wa wataalam kufanya Kazi kwa ufanisi mkubwa" amesema Ruyango
Hayo yamejiri wakati wa kikao cha Ushauri cha Wilaya hiyo(DCC) kwa upande wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru, ambapo wajumbe wamejadili maswala ya Elimu, biashara, afya, barabara, umeme na Maji. pia Mhe.Mhandisi Ruyango ametoa wito kwa jamii kujikinga dhidi ya maambukizi ya UVIKO-19 kwa kupata Chanjo sambamba na kuendelea kuchukua tahadhari.
Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Baadhi ya picha za tukio
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa