Afisa Mwandikishaji Jimbo la Arumeru Mashariki anawatangazia Wananchi waJimbo hilo kuwa, ameweka wazi daftari la kudumu la wapiga kura kwa siku nne kuanzia leo tarehe 17 hadi 20 June 2020.
WAHUSIKA
Wapiga Kura wote waliojiandikisha kwenye Daftari la kudumu la Wapiga Kura mwaka 2015 na wale waliojiandikisha wakati wa uboreshaji wa Daftari la kudumu la Wapiga Kura awamu ya kwanza na ya pili mwaka 2019 na mwaka 2020 .
Wapiga Kura ambao hawakuhakiki taarifa zao wakati wa uwekaji wazi Daftari la awali la Wapiga Kura.
Wapiga kura Watakao hakiki taarifa zao kwenye Daftari la awali la WapigaKura lililowekwa wazi na kukuta picha zao hazipo wanatakiwa kwendakituo cha Shule ya Msingi Leganga kilichopo Kata ya Usa River ili wachukuliwe picha na kupewa kadi nyingine.
MAMBO YA KUZINGATIA
Iwapo mpiga kura amehakiki taarifa na kutaka kufanya Marekebisho, atakiwa kwenda kituo cha Shule ya Msingi Leganga kilichopo Kata ya Usa River na kurekebisha taarifa zake.
Mpiga kura anayetaka kumwekea pingamizi mpiga kura asiye na sifa atatakiwa kwenda ofisi za Afisa mwandikishaji zilizopo Makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Mpiga kura anatakiwa kutoa taarifa za ndugu waliofariki ili waondolewe kwenye Daftari lakudumu la mpiga Kura.
Iwapo mpiga kura atahakiki taarifa zake na kubaini kuwa picha yake haipo, atatakiwa kwenda kituo cha Shule ya Msingi Leganga kilichopo Kata ya Usa River ili achukuliwe picha nyingine.
NJIA ZA KUHAKIKI TAARIFA ZA MPIGA KURA
Mpiga Kura atafika kwenye Kituo alichojiandikisha na kuhakiki taarifa zake kwenye orodha itakayobandikwa katika kituo hicho Kupiga simu ya kiganjani kwa kupiga na *152*00| na kufuata maelezo.
Mpiga kura atapiga simu namba 0800112100 na kufuata maelezo yatakayomuunganisha na mtoa huduma.
Mpiga kura anawezakutembelea tovuti ya Tume ya Taifa ya uchaguzi www.nec.go.tz na kubofya sehemu iliyoandikwa uhakiki.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa