Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mhandisi Richard Ruyango amewataka wakuu wa shule, watendaji wa Kata na Maafisa Elimu Kata na uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru kuhakikisha fedha za ujenzi wa miradi ya maendeleo kiasi cha Bilioni1.057 zilizogawiwa kwenye maeneo yao kuhakikisha zinatumika kwa uadilifu na uaminifu mkubwa ili kufikia azma ya Serikali ya kuboresha sekta ya elimu na afya na kuharakisha Maendeleo nchini.
Mhandisi Ruyango amesema hayo wakati wa kikao na Wakuu wa Idara na Vitengo , Wakuu wa Shule zilizopelekewa fedha , Watendaji wa Kata na Maafisa Elimu Kata kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo, ambapo amehimiza fedha hizo za miradi kutumika kama Serikali ilivyokusudia. " Tunamshukuru Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan kutuletea fedha Bilioni 1.057 za miradi , niwatake muwe waadilifu, waaminifu na wazalendo katika kutekeleza miradi hii na ikakamilike kwa wakati" amehimiza Ruyango
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Zainabu Makwinya amesema Halmashauri hiyo imenufaika kuletewa Bilioni 1.057 za ujenzi wa vyumba 17 katika shule 14 za Sekondari,ujenzi wa vyumba 9 vya madarasa katika shule 3 za msingi, ukamilishaji vyumba 6 vya madarasa katika shule sita za msingi, ujenzi wa nyumba nne za walimu (two in one) katika shule 4, ujenzi wa uzio wa shule ya msingi patandi ,ukamilishaji wa mabweni 4 katika shule nne za Sekondari, ujenzi wa bwalo moja na ukamilishaji wa nyumba moja ya mtumishi wa afya.
Naye, Mhe.Jeremia Kishili, mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru kwa niaba ya wananchi wa Halmashauri hiyo , ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kutoa fedha za miradi katika Halmashauri na kuhimiza wataalamu kutoa ushirikiano kwa wakati ili miradi ikamilike kwa wakati ambapo amehimiza ushirikiano baina na viongozi.
Kikao hicho cha uelewa wa pamoja kimefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru ambapo kimejumuisha Uongozi wa Halmashauri,Kamati ya Ulinzi na usalama Wilaya ya Arumeru,Wakuu wa Idara na Vitengo ,Watendaji wa Kata ,Wakuu wa Shule na Walimu wakuu wa shule zenye Miradi ambapo msisitizo umewekwa wa ukamilishaji miradi kwa wakati, uadilifu,weledi na uzalendo na uaminifu mkubwa katika kutekeleza miradi hiyo ya maendeleo.
Ikumbukwe katika fedha hizo zote kiasi cha shilingi Milioni 120 ni fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri ,Meru Kazi iendelee
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mhandisi Richard Ruyango akizungumza wakati wa kikao.
Mhe.Jeremia Kishili, mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru akizungumza wakati wa kikao.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Zainabu Makwinya akizungumza wakati wa kikao.
Wakuu wa Shule na Walimu wakuu wa zilizopelekewa fedha ,Watendaji wa Kata na Maafisa Elimu Kata wakato wa kikao.
Wakuu wa Idara na vitengo na wataalam wa sekta za ujenzi ,elimu nk wakati wa kikao
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa