Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhandisi, Richard Ruyango ameagiza miradi iliyoletewa fedha na Serikali kiasi cha Shilingi Bilioni 1.78 katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru kukamilika kabla ya tarehe 10 Desemba 2021 na kwa ufanisi mkubwa.
Mhe.Ruyango amesema hayo wakati wa kikao na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru ambapo amewataka kusimamia kwa karibu miradi hiyo na miradi yote iliyoletewa fedha na Serikali hivi karibu "nawataka msimamie fedha na utekelezaji wa miradi yote iliyoletewa fedha na Serekali kwa ufanisi mkubwa "amehimiza Ruyango
Ruyango amempongeza Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan kutoa Bilioni 1.4 fedha za mpango wa maendeleo dhidi ya UVIKO 19, kujenga vyumba 70 vya Madarasa katika Shule za Sekondari, Milioni 80(fedha za UVIKO -19) kujenga bweni la wanafunzi wenye mahitaji maalum katika Shule ya Msingi Patandi Maalum, Milioni 250 fedha za tozo za Simu kwaajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Mareu,na Shilingi Milioni 50(fedha za tozo) kwaajili ya ukamilishaji wa maboma 2 katika Shule za Sekondari
Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Zainabu Makwinya amemshukuru Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha hizo ambazo zimeshaingia katika akaunti za Shule na akaunti ya Zahanati ya Mareu na kuahidi kuzisimamia ili miradi hiyo kutekelezwa kwa ubora.
Baadhi ya picha za tukio.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhandisi Richard Ruyango ,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Zainabu Makwinya na Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Utawala na rasilimali watu .
Wakuu wa Idara na Vitengo wakati wa kikao
Wakuu wa Idara na Vitengo wakati wa kikao
Wakuu wa Idara na Vitengo wakati wa kikao
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa