Mkuu wa wilaya ya Arumeru, Mhandisi Richard Ruyango, ametoa siku 14 viongozi wa vijiji vya Kisimiri Juu, kata la Uwiro Halmashauri ya Wilaya ya Meru na kijiji cha Losinoni Kata ya Oldonyowasi, Halmashauri ya Arusha, kukaa vikao na kutoa mapendekezo ya maridhianao lengo likiwa kutatua mgogoro wa eneo la malisho katika Mlima Lekishori, eneo linalogombewa na wananchi wa pande hizo mbili.
Mhe.Ruyango ametoa agizo hilo baada ya kukutana na wananchi wa vijiji hivyo viwili kwa nyakati tofauti ambapo kila upande umeonyesha hauna shida na upande mwingine, lakini kila upande ukilalamikia upande mwingine kuwa, ndio chanzo cha mgogoro huo unaohusisha eneo hilo la malisho, linalodaiwa kutengwa miaka mingi iliyopita na wazee wao, kwa ajili ya malisho ya mifugo"Nawatoa siku 14, nendeni mkakae kila kila Kijiji na viongozi wake, mkalete mapendekezo ya maridhiano ya nini kifanyike ili kumaliza mgogoro huo, makubaliano hayo yawasilishwe ndani ya siku hizoo 14, kwaajili ya utekelezaji, lengo letu kubwa ni kumaliza mgogoro huu, ili wananchi waendelee kuishi kwa amani na utulivu,ameagiza Ruyango
Viongozi hao wa Vijiji wameweka wazi kuchoshwa na mgogoro huo ambao unawaumiza wananchi wa pande zote mbili kwani unarudisha nyuma maendeleo katika maeneo yao, kutokana na wananchi kutumia muda mwingi kwenye malumbano, badala ya kujikita kwenye shughuli za maendeo, pia umesababisha watu kupoteza mali zao,unahatarisha Maisha nk.
Katika mikutano hiyo, mkuu wa wilaya ya Arumeru aliambatana na mwenyekiti wa halmashauri ya Arusha, Mhe. Ojung'u Salekwa, mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, mkurugenzi mtendaji halmshauri ya Meru, Mwl.Zainabu Makwinya pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Arumeru.
Viongozi watakao husika kuandaa mapendekezo hayo ni pamoja na wawakilishi wa wananchi wakiwemo wenyeviti wa vijiji vya Losinoni Juu na Kisimiri Juu, Waheshimiwa Madiwani wa kata hizo mbili za Uwiro na Oldonyowasi, Maafisa watedaji wa vijiji na Kata zote mbili, Maafisa Tarafa wa Tarafa hizo mbili pamoja na viongozi wa mila.
BAADHI YA PICHA ZA TUKIO.
Mkuu wa wilaya ya Arumeru, mheshimiwa Mhandisi Richard Ruyango, akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kisimiri Juu kata ya Uwiro, Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Wananchi wa kijiji cha Losinoni Juu kata ya Oldonyowas wakati wa mkutano wa hadhara uliongozwa na mkuu wa wilaya ya Arumeru,
Mwananchi wa kijiji cha Kisimiri Juu kata ya Uwiro, akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliongozwa na mkuu wa wilaya ya Arumeru
Mkuu wa wilaya ya Arumeru, Mhandisi Richard Ruyango, akizungumza na viongozi wa mila 'Malaigwanani' wa vijiji vya Kisimiri Juu na Losinoni .
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa