Maafisa Watendaji wa Kata na Vijiji Katika Wilaya ya Arumeru wamepewa elimu na kukumbushwa kuzingatia Sheria,Taratibu na Kanuni (STK) zilizowekwa ili kutimiza wajibu wao katika maeneo yao ya kazi.
Elimu hiyo imetolewa katika kikao kazi cha Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Emmanuela Kaganda na Watendaji hao wanaojumuisha Halmashauri mbili za Arusha na Meru, kilichofanyika katika ukumbi wa shule ya Sekondari Fikiria kwanza iliyopo Kata ya Usariver Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Kikao hicho chenye lengo la kuwajengea uwezo Maafisa hao katika nyanja mbalimbali kama vile masuala ya usimamizi na matumizi ya Fedha za Umma, Ukusanyaji wa mapato na utoaji wa taarifa za mapato na matumizi, kuitisha Mikutano Mikuu, taratibu za utoaji wa vibali vya ujenzi, wajibu wa watendaji wa Kata na Vijiji katika mapambano dhidi ya Rushwa, pamoja na kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo yao.
Mkuu wa Wilaya hiyo, amesema kuwa kikao hicho kimelenga kuboresha utendaji kazi wa Watendaji wa Kata na Vijiji na baada ya elimu hiyo hatua zitachukuliwa kwa maafisa ambao hawatafuata maelekezo ya Serikali.
Arumeru ni yetu, tushirikiane kuijenga
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa