DC ARUMERU AWAPONGEZA WATALAMU MERU DC
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Emmanuela Kaganda ameupongza uongozi wa Halmashauri ya Meru, watalamu na Madiwani kwa kufanyakazi kwa ushirikiano, ambao matunda yake yanaonekana kwa halmashauri hiyo kwa kupata Hati Safi kwa miaka 3 mfululizo.
Mhe. Emmanuella ametoa pongezi hizo wakati akizungumza kwenye Mkutano Maalum wa Baraza la Madiwani wa kujadili Hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali za halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha 2022/2023, uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo leo Juni 14, 2024
Ameweka wazi kuwa, halmashauri ya Meru imeendela kufanya vizuri katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo ikiwa ni pamoja na usimamizi wa fedha za serikali unaozingatia viwango, na kuwezesha kupungua kwa kiasi kikubwa cha Hoja za ukaguzi ukilinganisha kwa miaka ya nyuma.
"Niwapongeze watalamu, waheshimiwa madiwani, viongozi wa Chama, wananchi wote wa Meru kwa umoja wenu kwa kuhakikisha, miradi inatekelezwa kwa wakati na kwa viwango vinavyotakiwa huku wananchi wakifurahia matunda ya serikali yao ya awamu ya sita chini ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani yenye malengo ya kusogeza huduma zote za kijamii kwenye maeneo yao" Amebainisha Mkuu huyo wa wilaya
Amewasisitiza watalamu na viongozi kuendelea kushirikiana ili kusukuma mbele gurudumu la maendeleo kwa kutekeleza ilani ya CCM yenye lengo la kufikisha huduma za jamii kwa wananchi, huduma zitakazotatua kero zao.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa