Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Eng.Richard Ruyango amewataka Viongozi na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru kuongeza ushirikianao na kuchapa kazi kwa bidii sambamba na kusikiliza na kutatua kero za wananchi.
Eng.Ruyango amesema ni muhimu kutatua migogoro ili kuharakisha maendeleo ambapo amewataka viongozi kuanzia ngazi ya Kitongoji hadi Wilaya kuhakikisha wanasikiliza na kutatua kero za wananchi kwenye maeneo yao .
Pia.Eng. Ruyango ametoa wito kwa wananchi kulinda amani na utulivu uliopo katika Wilaya hiyo ambapo amesisitiza hatamvumilia mtu yeyote atakaye jaribu kwa namna yoyote kuvuruga Amani iliyopo.
Haya yamejiri katika Kikao Kazi ambacho kimewajumuisha Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Kamati ya Ulinzi na Usalama, Taasisi za Serikali zilizopo Wilayani Arumeru, Maafisa Tarafa, Watendaji wa Kata na Vijiji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Eng.Richard Ruyango akizungumza wakati wa kikao Kazi
Mhe.Jeremia Kishili, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru akizungumza wakati wa kikao Kazi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Ndg.Emmanuel Mkongo akizungumzawakati wa Kikao.
Wakuu wa Idara/Vitengo ,Watumishi toka Taasisi za umma na Watendaji wa Kata/Vijiji wakati wa kikao kazi.
Wakuu wa Vitengo,Watendaji wa Kata/Vijiji wakati wa kikao kazi.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa