Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Emmanuela Kaganda ametoa wito kwa wananchi kuwa makini kwa kuchukua tahadhari katika kipindi hiki cha Mvua zinazoendelea.
Mhe.Kaganda amesema hayo wakati akizungumza na Wananchi eleo la Konoike Malula Halmashauri ya wilaya ya Meru ambapo imetokea ajali ya gari aina ya Noah iliyokuwa imebeba abiria watano kusombwa na maji ambaapo mpaka sasa miili minne imeokolewa na watu wawili akiwemo Dereva wa gari hiyo wameokolewa na wanaendelea kupata huduma za kiafya .
Aidha, Mhe Kaganda amesema Wilaya hiyo imepokea kwa huzuni kubwa tukio hilo ambapo ametoa pole kwa familia zilizo wapoteza wapendwa wao na kuwakumbusha wananchi kuenzi tamaduni za Mtanzania pale linapotekea tatizo badala ya kujikita kupiga picha.
Mhe.Kaganda amehimiza na kuwaasa waenda kwa miguu na wanaotumia vyombo vya moto kutokuingia kwenye maji yanayopita kwenye barabara au maeneo mengine bila kuchukua tahadhari kwani Dereva wa gari lililopata ajali Bw.Naiman Metili alijaribu kuvuka bila kujua nguvu ya maji.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa