Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro amepongeza juhudi zinazofanywa na Wauguzi katika utoaji bora wa huduma za afya.
Muro amesema hayo wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya utoaji vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya miaka 5 katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Amesema,Serikali imeboresha miundombinu katika sekta ya Afya kwa kujenga Hospitali ,vituo vya afya pamoja na kuhakikisha kunakuwa na upatikanaji wa dawa ambapo Wauguzi wanawajibu mkubwa kuchochea maendeleo hayo kwa hutoaji wa huduma bora.
Muro ametoa Wito kwa Wauguzi kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa weledi na ufanisi mkubwa "Serikali imeahidi kushughulikia stahiki za watumishi ,natoa rai kwenu kuchapa kazi kwa maendeleo ya Taifa"amehimiza Muro
Aidha Muro amewaelekeza Wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha wanalipwa stahiki za watumishi ambazo hazina ulazima wa kusubiri.
Ikumbukwe leo ni maadhimisho ya siku ya Wauguzi.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa