Mkuu wa Wilaya ya Arumeru ,Mkoani Arusha, Ndg. Jerry Muro ameagiza kusimamishwa kwa shughuli zote za kilimo na ufugaji kwenye Msitu wa Jamii wenye ukubwa wa Hekari zaidi ya Elfu mbili uliopo Kata ya Uwiro Halmashauri ya Wilaya ya Meru .
Muro ametoa agizo hilo wakati wa ziara yake ya kushtukiza kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero na changamoto zinazowakabili wananchi wa wilaya ya Arumeru, ikiwa ni sehemu ya Agenda yake kwa mwaka 2020 kabla ya uchaguzi mkuu mwezi October 2020.
Aidha baada ya kubaini uharibifu mkubwa uliosababishwa na shughuli za kilimo na ufugaji kwenye Msitu huo wenye zaidi ya Hekari Elfu Mbili amesema Serikali haipo tayari kuona eneo hilo linakuwa jangwa hivyo amezuia eneo hilo kutumika kwa shuguli za kibinadamu kwa kipindi cha Miaka miwili.
Wananchi wa na Viongozi wa Kata ya Uwiro wamempongeza Mkuu wa Wilaya ya Arumeru kwa kuzuhia uharibufu wa eneo hilo kwani itasaidia kurejesha uoto wa asili.
Aidha ziara hiyo ya Muro ambayo ni katika Kata zote 56 za Wilaya ya Arumeru.
Eneo hilo la jamii kwa Sasa litakuwa chini ya Uangalizi wa NGO ya Soledaridad.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa