Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Mwinyi Ahmed Mwinyi mapema hii Leo amehitimisha Mafunzo ya JKT Mujibu wa Sheria kikosi Cha 833kj Oljoro Oparesheni Nishati Safi.
Katika hafla hiyo Mhe. Mwinyi amewataka vijana hao waliomaliza Mafunzo Yao kukiishi kiapo Chao na kuwa mabalozi wazuri na wema kwa nchi Yao.Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Mwinyi Ahmed Mwinyi amewataka wahitimu wa Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa Kikosi Cha Jeshi 833 kuhakikisha Mafunzo waliyopatiwa yanakwenda kuwa tija kwa Taifa na kutorubuniwa na vikundi au kikundi flani kwa maslai Ovu
Aidha ameendelea kumshukuru na kumpongeza Dkt. Samia Suluhu Hassani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuruhusu na kuweka miundombinu Bora yakuendele kulea na kuwa weka vijana katika Hali ya kizalendo na nchi Yao.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa