Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhandisi Richard Ruyango atoa wito kwa Madiwani na Wataalum wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru kushirikiana kikamilifu katika utekelezaji wa shughuli za Serikali kwa maendeleo ya Halmashauri hiyo.
Ruyango ameyasema hayo wakati wa Mkutano wa Baraza la Madiwani ambapo amehimiza kuwa Halmashauri inajengwa na Madiwani na Wataalamu. Hivyo ameelekeza taarifa zinazowasilishwa kwenye baraza hilo kutoka kwenye kata kuwa na uhalisia ili kuepuka hoja zisizo na msingi, "taarifa hizi ni Kumbukumbu za Kudumu za Halmashauri, hivyo ni lazima ziwe sahihi "amehimiza Ruyango.
Naye,Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mhe.Jeremia Kishili amewataka Madiwani kupitia taarifa zao za kata kabla ya kuziwasilisha kwaajili ya baraza .Pia katika changamoto ya uharibifu wa wanyama pori Mhe.Kishili ameitaka idara ya maliasili kutoa elimu kwa wananchi juu ya kuepuka madhara ya wanyama pori.
Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Zainabu Makwinya amewaelekeza Watendaji wa kata kuhakikisha taarifa zinazotoka kwenye maeneo yao ni sahihi ambapo pia amewashukuru Waheshimiwa Madiwani ,wakuu wa Idara na Vitengo kwa ushirikiano mzuri wakati wa kikao na kuwasihi kuendelea hivyo .
Vilevile Mwl.Makwinya amemshukuru Mhe.Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kumteua kuwa mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru ambapo pia ametuma Salaam za shukurani kwa viongozi na watumishi wa Halmashauri ya Chalinze alipofanya nao Kazi kwa miaka sita akiwa na cheo Cha Mkuu wa Idara ya elimu Msingi.
Mkutano huo wa baraza umekamilika kwa Siku ya kwanza ambapo miongoni kwa ajenda zake ni pamoja na uwasilishaji wa taarifa za utekelezaji za kata kwa kipindi cha Aprili hadi Juni 2021.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhandisi Richard Ruyango akizungumza wakati wa Mkutano wa Baraza la Madiwani.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mhe.Jeremia Kishili akizungumza wakati wa Mkutano .
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Zainabu Makwinya akizungumza katika Mkutano wa Baraza la Madiwani.
Waheshimiwa Madiwani wakati wa Mkutano.
Waheshimiwa Madiwani wakati wa Mkutano.
Waheshimiwa Madiwani wakati wa Mkutano.
Waheshimiwa Madiwani wakati wa Mkutano.
Waheshimiwa Madiwani wakati wa Mkutano.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa