Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru ,Ndg.Emmanuel Mkongo ametoa wito kwa wadau wanaotoa huduma ya elimu kutoa Elimu itakayoletatija kuelekea uchumi wa Kati .
Mkongo amesema hayo wakati wa maafali ya 18 ya wanafunzi wanaotarajia kuhitimu kidato cha nne mwaka huu katika Shule ya Sekondari ya kisabato Tanzania TASS inayomilikiwa na dhehebu la Kisabato iliyopo katika Halmashauri ya Meru .
Aidha, Mkongo ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali hayo,amesema Serikali ya Awamu ya tano imeweka mipango ya kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025 kupitia uchumi wa viwanda unaotegemea Sayansi na Teknologia ,hivyo katika kutekeleza Ilani ya chama cha Mapinduzi CCM ,ibara ya 52 inayoelekeza Serikali kuboresha Elimu, Serikali inahakikisha watoto wa kitanzania wanapata elimu kuanzia ngazi ya awali mpaka elimu ya juu ambapo kwa mwaka wa fedha 2019/2020 Serikali imetenga bilioni 288.5 kwaajili ya elimu bila malipo kwa shule za msingi na Sekondari,uboreshaji wa sekta ya Elimu umeongeza kwa kiasi kikubwa cha ufaulu ambapo Shule ya Sekondari ya Kata Kisimiri iliyopo katika Halmashauri hiyo imeongoza kwa kushika nafasi ya kwanza kitaifa katika matokeo ya kidato cha sita mwaka 2019.'Haya ni mafaniko makubwa ya Serikali ya awamu ya Tano kwa Shule ya Kisimiri ambayo ni ya Kata kufanya vizuri kuliko shule kongwe na za binafsi Nchini"amesisitiza Mkongo.
Aidha Mkongo amewasisitiza wahitimu hao kusoma kwa bidii na waweze kupata sifa ya kuchaguliwa kwa masomo ya Fizikia, Kemia, Hesabu na masomo ya sanaa, kujiunga kidato cha tano katika Shule hiyo Kinara Nchini, kwani Serikali huchagua wanafunzi kujiunga na shule zake bila ubaguzi kwa lengo la kujenga taifa moja na kudumisha umoja na mshikamano .
Mkongo amesema uboreshaji wa Elimu unaenda sambamba hadi ngazi ya elimu ya juu ambapo Serikali hutoa mkopo kwa wanafunzi wanaokidhi vigezo waliosoma katika Shule ya Serikali au Binafsi ,ambapo kwa mwaka huu wa fedha 2019/2020 Serikali imetenga Shilingi Bilioni 450 kwa ajili ya kutoa mikopo kwa wanafunzi watakaojiunga na Elimu ya juu watakaokidhi vigezo.
Mkongo amesisitiza kuna haja ya wadau wanao toa huduma ya elimu kuongeza juhudi ya kutoa elimu inayojikita katika Sayansi na teknolojia ili kuandaa nguvu kazi yenye ujuzi mahususi kwaajili ya uchumi wa viwanda kwakuwa kuna uhitaji mkubwa wa vijana wabunifu na wajuzi katika kuelekea uchumi wa kati.
Akihitimisha Mkongo amewaasa wahitimu hao 29, kufanya maandalizi kwa muda uliobakia ili waweze kufanya vizuri katika mtihani wa kuhitimu kidato cha nne utakaofanyika kuanzia tarehe 04 hadi 22 Novemba 2019,pia amewataka wanafunzi wote kuwa na nidhamu na uadilifu ili waweze kufanya vizuri katika masomo yao .
Mkuu wa Shule hiyo Ndg. Borega Petro akisoma taarifa ya shule hiyo ameeleza kuwa shule hiyo mbali na kutoa Elimu imekuwa ikiwandaa kiroho na kiakili wanafunzi wake kuwa Raia mwema na watakao kuwa waadilifu na wazalendo..
Maafali hayo yamefanyika katika viwanja vya shule Hiyo iliyopo Kata ya Ngongongare karibu na Chuo kikuu cha ARUSHA,
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru ,Ndg.Emmanuel Mkongo akizungumza wakati wa maafali Shule ya Sekondari TASS
Mkuu wa Shule ya TASS Ndg. Borega Petro akisoma taarifa ya shule hiyo.
Wahitimu wakisoma Risala
Wahitimu wakati wa Maafali.
Mgeni Rasmi ,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru akikabidhi cheti kwa mhitimu .
Wazazi na walezi wakati wa maafali katika Shule ya TASS.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa