Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Zainabu Makwinya amewataka mafundi wanaotekeleza miradi ya EP4R katika Halmashauri hiyo kuwa na kasi ya ujenzi wa miradi hiyo bila kuathiri uimara .
Mwl.Makwinya ameelekeza hayo wakati wa ziara yake katika Shule ya Msingi Kisimiri chini,Kata ya Uwiro ambapo ujenzi wa mradi wa vyumba viwili vya Madarasa ya EP4R umeonekana kuwa wa polepole kutokana na fundi kutokuwa na Nguvu kazi ya kutosha na kutokuwepo eneo la mradi .
Aidha, Mwl.Makwinya ameuelekeza Uongozi unaosimamia ujenzi huo kutafuta Suluhu Mara moja ili mradi huo kukamilika kwa wakati kama ilivyokusudiwa.
Vilevile Makwinya alitembelea na kupongeza ari ya ujenzi wa vyoo vya matundu 12 vya muundo wa SWASH katika Shule hiyo pamoja na mradi wa uchimbaji Maji yatakayo sambazwa kwenye Shule ya Sekondari Kisimiri.
Diwani wa Kata ya Uwiro Mhe.Dauson Urio ameishukuru Serikali kupeleka miradi ya vyumba vya Madarasa mawili ya EP4R na Vyoo hivyo vya matundu 12 ,pia amehimiza Kazi za ujenzi wa miradi kutolewa kwa mafundi wanaojituma zaidi.
Kata ya Uwiro ni Miongoni mwa Kata saba(7) ambazo Mkurugenzi Zainabu amefanya ziara ya kukagua na kutembelea utekelezaji wa miradi ya EP4R ,Miradi ya Nguvu za wananchi na michango ya wahisani,miradi ya TASAF pamoja na maboma ya mda mrefu ,ambapo aliambatana na Afisa Elimu Sekondari pamoja na Wahandisi wa Ujenzi toka Halmashauri.
Diwani wa Kaya ya Uwiro Mhe.Dauson Urio (wa kwanza Kulia) pembeni yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Zainabu Makwinya wakikagua msingi wa vyumba 2 vya madarasa ya EP4R Katika Shule ya Msingi Kisimiri Chini.
Ujenzi wa vyoo vya matundu 12 vya muundo wa SWASH
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa