• Barua pepe |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
Meru District Council
Meru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Meru

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, Takwimu na Ufatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Utumishi na Utawala
      • Usafi na mazingira
      • Ardhi na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Manunuzi na ugavi
      • Uchaguzi
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Misitu
    • Ufugaji wa Ngombe wa Maziwa
    • Ujenzi wa Kituo cha Biashara
    • Ujenzi wa Eneo la Mapumziko
    • Ujenzi wa kituo cha Mabasi cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Malori cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Michezo
    • Kilimo cha Nyanya
    • Ufugaji wa Nyuki
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • AIDS
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Miongozo
    • Fomu mbalimbali
    • Utaratibu
  • Kituo cha habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

MKURUGENZI MERU AAGIZA UJENZI WA MADARASA KWENDA SAMBAMBA NA UTENGENEZAJI WA VITI,MEZA

Imewekwa: November 28th, 2021

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Zainabu Makwinya ameagiza kasi ya ujenzi wa vyumba 70 vya Madarasa ya Uviko-19 kwenda sambamba na utengenezaji wa viti na meza.

Mwl.Makwinya ametoa agizo hilo wakati wa ziara ya ufuatiliaji wa ujenzi wa vyumba vya Madarasa hayo ambapo ametembelea ujenzi wa vyumba vya Madarasa katika shule nane(8) za Sekondari na kubaini nguvu kubwa kuwekezwa kwenye ujenzi wa Madarasa pekee "niwaelekeze Wakuu wa Shule, timu za ufuatiliaji na walezi wa Kata kuhakikisha ujenzi wa Madarasa unakwenda sambamba na utengenezaji wa viti na meza" ameagiza Makwinya

Vilevile Mwl.Makwinya amesema Miradi mingi imefikia hatua ya ufungaji wa lenta na upauzi, hivyo ameelekeza kwa miradi ambayo kasi yake ni ndogo Wakuu wa Shule  kuhakikisha miradi hiyo inatekelezwa kwa kasi zaidi ikiwa ni pamoja na  fundi kuwa na vibarua wa kutosha.

Aidha katika Ziara hiyo Mkurugenzi.Zainabu amekagua ujenzi wa Vyumba vya Madarasa katika shule za Sekondari, Momela, Umoja King'ori, Miririnyi, King'ori, Maruvango, Nkoasenga ,Nasholi pamoja na ujenzi wa Zahanati ya Mareu na bweni katika Shule ya Sekondari Nkoasenga .

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Meru (kilemba kichwani)  wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa vyumba viwili (2) vya madarasa Shule ya Sekondari Momela,mradi unaogha rimu Tsh.Milioni 40, fedha za UVIKO -19

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru  wakati wa ukaguzi wa ukamilisha wa maboma ya madarasa(2) Shule ya Sekondari Umoja King'ori,mradi unaogharimu Tsh.Milioni 50, fedha za Tozo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya  Meru  wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa vyumba viwili (2) vya madarasa Shule ya Sekondari Miririnyi,mradi unaogharimu Tsh.Milioni 40, fedha za UVIKO -19

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Meru wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa vyumba viwili (2) vya madarasa Shule ya Sekondari King'ori,mradi unaogharimu Tsh.Milioni 40, fedha za UVIKO -19

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Meru  wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa Chumba kimoja (1) Cha  darasa Shule ya Sekondari  Nkoasenga,mradi unaogharimu Tsh.Milioni 20, fedha za UVIKO -19


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Meru wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa Bweni la Wanafunzi wa kike katika Shule ya Sekondari Nkoasenga, Ikiwa ni mchango wa wadau kuunga mkono uboreshaji wa miundombinu ya sekta ya elimu unaofanywa na Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan.


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya  Meru  wakati alipotembelea na  kukagua ujenzi wa Zahanati ya Mareu unaogharimu Milioni 250 fedha za tozo.


Matangazo ya Kawaida

  • KUITWA KWENYE USAILI October 28, 2024
  • KUITWA KWENYE USAILI June 24, 2024
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MTAALA WA ELIMU YA AWALI NA MSINGI 2022. February 18, 2022
  • UUZAJI WA VIWANJA ENEO LA NGURUDOTO LIMEANZA. November 27, 2018
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • AJIRA MPYA MERU DC WAPATIWA MAFUNZO

    April 02, 2025
  • NAIBU WAZIRI MAENDELEO YA JAMII,JINSIA WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUMU AKAGUA MIRADI YA S.O.S

    March 15, 2025
  • MAFUNZO YA MFUMO WA TAUSI MERU DC YAFUNGWA

    February 15, 2025
  • TAHAPAO NA MERU DC WAWEKA NGUVU KWENYE KAMATI ZA MTAKUWA

    February 19, 2025
  • Tazama Vyote

Video

ELIMU YA KUKABILIANA NA TAHADHARI YA MVUA ZA EL NINO YAANZA KUTOLEWA HALMASHAURI YA MERU.
Video Zaidi

Viungo Haraka

  • Kupata Salary Slip
  • Sheria ndogo za Halmashauri ya Wilaya ya Meru

Kiungo Kuhusiana

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Utumishi
  • Watumishi Portal
  • Tovuti ya Mkoa wa Arusha
  • Ajira Portal
  • Government Salary Slip Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Meru

    Anwani: P.o. Box 462 Usa River

    Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@merudc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa