Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl. Zainabu J. Makwinya akichangia kutoa ufafanuzi wa maswali yaliyoulizwa na Walimu katika kikao cha Walimu na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dr. Charles E. Msonde Katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru .
Mkurugenzi Makwinya ameeleza kuwa katika ziara zake za kutembelea miradi ya Maendeleo ameweka utaratibu wa kusikiliza kero na changamoto mbalimbali za walimu na watendaji katika Kata anazopita.
" Nimeweka utaratibu wa kusikiliza kero na changamoto mbalimbali za watumishi katika Kata zao na kuwaelekeza waniandikie na kuziwasilisha ofisini kwangu moja kwa moja na mimi kuzielekeza kwa Afisa Utumishi na Mkaguzi wa Ndani kama ni masuala yanayohusu madai ya fedha mbalimbali ili kuweza kuzifanyia kazi." amesema Makwinya.
Aidha, Mkurugenzi Makwinya ameeleza kuwa idadi ya watumishi wa Halmashauri ya Meru wakiwemo na walimu wanaodai madai mbalimbali kama vile mapunjo ya mishahara kwa mwaka 2021 hadi 2023 wamelipwa watumishi 1,048 zaidi ya shilingi Bilioni 1.3.
Vilevile imeelezwa kuwa kwa mshahara wa mwezi huu wa tano, walimu 372 wanatarajiwa kupanda daraja la mserereko na 1,125 watapanda madaraja.
Katika hatua nyingine, Mwl. Makwinya ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuleta Fedha nyingi za utekelezaji wa miradi ya maendeleo lakini pia kulipa madeni ya watumishi yaliyosimama kwa kipindi kirefu takribani zaidi ya miaka mitano.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa